Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 24 January 2012

Siku kama ya leo da'Nancy Alizaliwa!!!!!!

Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita,Da'Nancy Bibi ya Nyotu Alizaliwa!!!
Tunakutakia kila la kheri na baraka katika maisha yako,Mungu azidi kukubariki sana,
Upendo,Utu wema,Fadhili,Busara,Ucheshi na Mengine mengi Mungu amekujalia dada Nancy.
Wewe ni Rafiki wa nyakati zote kwa shida na Raha,Kupitia wewe nimejifunza meeengi sana sana.
Uwe na wakati mwema kila iitwapo Leo.
Familia ya Isaac Tunakupendaaa na kukuthani sanasana sana.
Mungu awe nasi Daima.




Wednesday 18 January 2012

Ulale kwa Amani da'Regia!!!!!



 Poleni sana Ndugu,Jamaa,Marafiki na Taifa pia.Bwana alitoa na Bwana Ametwaa.

Monday 16 January 2012

Utafiti;Eti kuangalia TV kwa saa Moja kunapunguza dakika22 za Maisha Yako!!!


  • Ukifuata kila linalosemwa na wanasayansi utashindwa kuishi. Leo watasema kunywa kahawa kunapunguza msongo wa mawazo. Kesho watasema kunywa kahawa  huko huko kunaongeza shinikizo la damu na uwezekano wa kupata pigo la kiharusi. Leo watasema hiki na kesho watasema kile ali mradi ni vurugu tupu. Kibaya zaidi ni ukimya wao kuhusu nini cha kufanya hasa pale tafiti zao zinapotoa matokeo yanayokinzana
  • Kwa vile nyingi ya tafiti hizi hufanyika huko Ulaya na Marekani, Waafrika inabidi kuyapokea matokeo ya tafiti hizi kwa uangalifu sana kwani huwa hayazingatii mazingira yetu na mtindo wetu wa maisha (japo sasa tunajitahidi sana kuwaiga kwa kila kitu).  
  • Utafiti uliofanywa mwaka jana na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Queenesland unaonyesha kwamba kuangalia runinga kwa watu wenye umri wa miaka 25 na kuendelea kuna madhara makubwa kiafya na kunapunguza muda wa kuishi. Utafiti huu unaonyesha kwamba kwa kila saa moja unayoitumia ukiangalia runinga basi unajipunguzia dakika 22 katika maisha yako. Hii ni sawa na kuvuta sigara mbili. 
  • Wanasayansi hawa wanasema kwamba tatizo hasa siyo kuangalia tv bali madhara ya kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ambako kunasababisha magonjwa ya moyo, kisukari, kunenepeana na matatizo mengine ya kiafya yanayosababishwa na mtindo wa maisha ya kubweteka (sedentary lifestyle). Kufanya mazoezi, hata kama ni dakika 15 tu kwa siku ni jambo la muhimu na kumeonyeshwa kuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza siku tatu katika maisha yako.
              Kusoma zaidi habari hii ingia kwa  Blog ya kaka Matondo[MMN]http://www.matondo.blogspot.com
                                   Ahsante kaka Matondo.

Saturday 14 January 2012

Siku kama ya leo kaka Isaac Alizaliwa!!!!!!

Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita, Kaka Isaac, babake  Sandra na Tracey,Mume ya MadameRachel-siwa,Alizaliwaaa!!!
Tunamshukuru sana Mungu kwa yote juu yako,Mungu akubariki na kukulinda kila inapoitwa Leo.
Akuongezee Miaka Mingi na Ufanikishe malengo yako.Uzidi kuwa Baraka kwetu na Kwa Watu wote.
 Tunakupenda saaana,Wako Rachel,Sandra,Tracey[ Rasca].