(Lifestyle)Jamii,Tamaduni ,Matukio,Maisha ya Waswahili. Wapendao Kiswahili/Waswahili,Marafiki wa Swahili na Waswahili, Na Mengineyo ya Karibu, Yahitajikayo Kujuzwa Waswahili.Karibuni sana!!!!!!!
Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
kuona post ingia hapa; http://swahilinawaswahili.blogspot.com/2011/06/wanaume-na-mitindoleo-wenye-rasta-eti.html?showComment=1478354804495#c4462530939513813249"Wanaume na Mitindo,Leo wenye Rasta Eti!!!!!!!": hizo sio Rasta, hivyo ni vishungi/vifundo ama dread kwa kizungu. Rasta ni kifupisho cha Rastafarian ambayo ni imani inayoamini kwamba mfalme Haile Selasie ndiye Masihi/masiya (Ras Tafar ni jina halisi la Haile selasie kabla ya kuwa mfalme, alipewa jina la haile selasie lenye maana ya 'nguvu ya utatu mtakatifu' mara baada ya kushika ufalme wa ethiopia, hii ni sawa na mapapa wa kanisa katoliki hupewa majina mengine kama vile John, benedict, baada ya kupewa u-papa). Rastafarians huamini kwamba bustani ya Eden iko ethiopia kwani ufafanuzi wake kwenye kitabu cha MWANZO unatoa ushahidi kuwa ni ethiopia kwani jina KUSH limetajwa (soma Mwanzo kwa uhakika zaidi) vile vishungi vya nywele hufugwa muumini wa Rastafari anapoingia kwenye nadhiri ya kumtumikia Mungu kwenye maisha yake yote (rejea jinsi samson wa kwenye biblia alivyowekewa nadhiri ya kumtumikia Mungu na kuamriwa kutonyoa nywele)
Posted by Ras choyo to Swahili na Waswahili at 5 November 2016 at 14:06 Asante kwa mawazo/mchango wako kaka Ras Choyo "Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.