Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 24 May 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 132...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Lakini nyinyi ndio watu aliowakomboa kutoka Misri katika tanuri la chuma. Aliwatoeni huko ili muwe watu wake kama vile mlivyo hivi leo.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kwa sababu yenu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alinikasirikia, akaapa kwamba mimi sitavuka mto Yordani kuingia katika nchi ile nzuri anayowapeni iwe mali yenu. Mimi nitafia katika nchi hii wala sitauvuka mto, lakini nyinyi mko karibu kuuvuka na kwenda kuimiliki nchi ile nzuri.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Jihadharini sana msije mkasahau agano ambalo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amefanya nanyi; msijifanyie sanamu ya kuchonga katika umbo la kitu chochote ambacho Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewakataza kumfananisha, maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ni moto uteketezao; yeye ni Mungu mwenye wivu.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

Sifa ya nyumba ya Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1Ee Mwenyezi-Mungu, mkumbuke Daudi,
kumbuka taabu zote alizopata.
2Ukumbuke ahadi aliyokupa, ee Mwenyezi-Mungu,
kiapo alichokuapia, ewe Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3“Sitaingia ndani ya nyumba yangu,
wala kulala kitandani mwangu;
4sitakubali kulala usingizi,
wala kusinzia;
5mpaka nikupatie wewe Mwenyezi-Mungu mahali pa kukaa,
makao yako, ewe Mwenye Nguvu wa Yakobo!”
6Huko Efratha tulisikia habari za sanduku la agano,
tukalikuta katika mashamba ya Yearimu.
7“Haya! Twende nyumbani kwa Mungu,
tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!”
8Inuka ee Mwenyezi-Mungu, nenda kwenye maskani yako;
inuka pamoja na sanduku la agano la uwezo wako!
9Makuhani wako wawe waadilifu daima;
na waaminifu wako wapige vigelegele vya furaha!
10Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako,
usimkatae huyo mfalme uliyemweka wakfu.
11 Taz Zab 89:3-4; Mate 2:30 Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi kiapo thabiti,
kiapo ambacho hatakibatilisha:
“Nitamtawaza mmoja wa wazawa wako mwenyewe,
kuwa mfalme baada yako.
12Watoto wako wakishika agano langu,
na kuzingatia mafundisho nitakayowapa,
watoto wao pia watakuwa wafalme kama wewe.”
13Mwenyezi-Mungu ameuchagua mji wa Siyoni,
ametaka uwe makao yake:
14“Hapa ndipo nitakapokaa milele,
ndipo maskani yangu maana nimepachagua.
15Nitaubariki sana mji wa Siyoni kwa mahitaji yake;
nitawashibisha chakula maskini wake.
16Nitawafanikisha makuhani wake kwa wokovu;132:16 … kwa wokovu: Mstari huu wa kwanza wa aya hii haueleweki; wengine wana ushindi badala ya wokovu.
waaminifu wake watapiga vigelegele vya furaha.
17Humo nitamchipusha mfalme shujaa wa ukoo wa Daudi:
Kama taa iwakayo nitamtegemeza mfalme niliyemteua.
18Maadui zake nitawavika aibu;
lakini yeye nitamvika fahari ya kifalme.”

Zaburi132;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: