Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 5 March 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 74...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante

 kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!

Basi, inaposemwa: “Alipaa juu,” ina maana gani? Maana yake ni kwamba, kwanza alishuka mpaka chini kabisa duniani. Basi, huyo aliyeshuka hapa duniani ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote apate kuujaza ulimwengu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.....


Ndiye aliyewapa watu zawadi: Wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe waeneza Injili, wengine wachungaji na waalimu. Alifanya hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo, na hivyo sote tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila. Kama tukiuzingatia ukweli kwa moyo wa mapendo tutakua katika kila jambo kulingana na Kristo ambaye ndiye kichwa; chini ya uongozi wake, viungo vyote vya mwili hushikamana pamoja, na mwili wote hutegemezwa kwa msaada wa viungo vyake. Basi, kila kiungo kikitekeleza kazi yake ipasavyo, mwili wote hukua na kujijenga katika upendo.
Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

Ombolezo juu ya kubomolewa hekalu
(Utenzi wa Asafu)
1Kwa nini, ee Mungu, umetutupa kabisa?
Mbona hasira yako inawaka dhidi ya kondoo wako!
2Kumbuka jumuiya yako uliyojipatia tangu kale,
kabila ulilolikomboa liwe mali yako,
kumbuka mlima Siyoni mahali unapokaa.
3Pita juu ya magofu haya ya kudumu!
Adui wameharibu kila kitu hekaluni.
4Maadui zako wamenguruma ushindi hekaluni mwako!
Wameweka humo bendera zao za ushindi!
5Wanafanana na mtema kuni,
anayekata miti kwa shoka lake.74:5 aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
6Waliivunjavunja milango ya hekalu,
kwa mashoka na nyundo zao.
7Walichoma moto patakatifu pako;
walikufuru mahali pale unapoheshimiwa.
8Walipania kutuangamiza sote pamoja;
walichoma kila mahali tulipokutania kukuabudu nchini.
9Hatuzioni tena ishara zetu takatifu,
hatuna tena nabii yeyote!
Hata hatujui yatakuwa hivi hadi lini!
10Mpaka lini, ee Mungu, adui atakucheka?
Je, watalikufuru jina lako milele?
11Mbona umeuficha mkono wako?
Kwa nini hunyoshi mkono wako?
12Hata hivyo wewe Mungu ni mfalme wetu tangu kale;
umefanya makuu ya wokovu katika nchi.
13Kwa enzi yako kuu uliigawa bahari;
uliviponda vichwa vya majoka ya bahari.
14 Taz Zab 104:26 Wewe uliviponda vichwa vya dude Lewiyathani;
ukawapa wanyama wa jangwani mzoga wake.
15Wewe umefanya chemchemi na vijito;
na kuikausha mito mikubwa.
16Mchana ni wako na usiku ni wako;
umeweka mwezi na jua mahali pao.
17Wewe umeweka mipaka yote ya dunia;
umepanga majira ya kiangazi na ya baridi.
18Kumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, madharau ya maadui zako;
taifa pumbavu linalikashifu jina lako.
Sisi ni dhaifu kama njiwa.
19Usiwatupie wanyama wakali uhai wa wapenzi wako;
usiyasahau maisha ya maskini wako.74:19 Kiebrania: Roho ya njiwa wako; lakini yawezekana kwamba mwandishi alikuwa anafananisha udhaifu wa watu na njiwa! Kwa maana hiyo roho ya njiwa wako na maisha ya maskini wako ni sambamba.
20Ulikumbuke agano ulilofanya nasi!
Nchi imejaa uharamia kila mahali pa giza.
21Usiwaache wanaokandamizwa waaibishwe,
uwajalie maskini na wahitaji walisifu jina lako.
22Inuka, ee Mungu, ukajitetee;
ukumbuke wanavyokudharau kila siku watu wasiokujua.
23Usisahau makelele za maadui zako;
na ghasia za daima za wapinzani wako.


Zaburi74;1-23

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: