Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana? Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mungu wetu,Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo ni mali yako,Hata sisi ni mali yako Baba,Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.. Asante kwa wema na fadhili zako Mungu wetu.. Asante kwa ulinzi wako wakati wote Yahweh..! Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Mngu wetu.. Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu.. Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea.. Baba wa Mbinguni utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote.. Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike kwa Damu ya Mwanao Mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti . Yeye aliteseka ili sisi tupate kupona.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukapate kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi.. Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako tunaomba utubariki na kubariki kazi zetu,Biashara,Masomo,tuingiapo/tutokapo,vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri na tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahaweh.. Ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo.. Tazama wenye shida/tabu, wanapoitia magumu/majaribu mbalimbali,waliokatika vifungo mbalimbali Mungu wetu ukawaguse na mkono wako wenye nguvu ukawaponye na kuwaokoa katika mapito yao..
Wapendwa/Waungwana; Mungu akatupe Kibali Leo na wakati mwingine cha kuwaombea Ndugu/jamaa zetu na watu wengine..
Jehovah tunaweka nyumba zetu,familia,ndugu,jamaa na wote wanaotufahamu kwa namna moja au nyingine na wote wanaosoma hapa..
Baba wa Mbingu tunaomba ukatulinde na kutuokoa,ukatuponye kiroho na ukatupe amani ya moyo, ukatujenge kiroho/kiimani,tukaijue kweli yako na kukufuata wewe Mungu na kufuata sheria zako,Agano lako na Amri zako..Ukatufadhili ee Mungu wetu na kutuhurumia,Ukatusamehe na ukatuepushe na Hasira,Chuki,Wivu,Tamaa,Masimango,Kujisifu/kujikweza, kisasi na yote yasiyo kupendeza wewe..
Ee Mungu wetu ukatuinue na kutusimamisha, tazama ndugu zetu walio asi Mungu wakurudie pasipo na aibu wakapate Nuru na Mwanga kwenye maisha yao...
Lifuatalo ni simulizi la Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa, nilipokuwa katika mji mkuu wa Susa, katika mwezi wa Kislevu wa mwaka wa ishirini, Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akaja pamoja na baadhi ya watu toka nchini Yuda. Nikawauliza kuhusu Wayahudi wenzetu waliosalimika, yaani ambao hawakuhamishiwa Babuloni na kuhusu mji wa Yerusalemu. Wao wakaniambia, “Wayahudi waliosalimika na kubaki katika mkoa ule, wako katika taabu na aibu. Ukuta wa mji wa Yerusalemu umebomolewa na malango yake yameteketea.” Niliposikia hayo nilikaa chini na kulia, nikaomboleza kwa siku kadhaa. Nikafunga na kumwomba Mungu wa mbinguni, nikisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa mbinguni, wewe u Mungu aliye mkuu na wa kutisha, unalishika agano lako na unawafadhili wale wakupendao na kuzishika amri zako. Yasikilize kwa makini maombi yangu, na uniangalie mimi mtumishi wako, ninapokuomba kwa ajili ya watumishi wako, watu wa Israeli, usiku na mchana. Ninaungama dhambi za watu wa Israeli, tulizofanya mbele yako. Mimi pamoja na watu wa jamaa yangu tumefanya dhambi. Tumetenda mabaya mbele yako, hatujazishika amri zako, kanuni na maagizo yako uliyomwagiza mtumishi wako Mose. Kumbuka sasa lile ulilomwambia mtumishi wako Mose, uliposema, ‘Kama hamtakuwa waaminifu, nitawatawanya miongoni mwa mataifa. Lakini mkinirudia, mkazishika amri zangu na kuzifuata hata ingawa nitakuwa nimewatawanya mbali kabisa, nitawarudisha mahali nilipochagua kuwa mahali pangu pa kuabudiwa.’ Watu wa Israeli ni watumishi wako na watu wako uliwakomboa kwa uwezo wako na mkono wako wenye nguvu. Ee Bwana, yasikie maombi yangu mimi mtumishi wako na ya watumishi wako wanaofurahia kukutii wewe. Nakuomba unifanikishe leo, mimi mtumishi wako, na kunijalia kuhurumiwa na mfalme.” Basi, mimi nilikuwa na jukumu la kumpa mfalme kinywaji.
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu na ukatupe sawasawa na mapenzi yako
ee Mungu wetu na ukasikie kulia kwetu na kupokea maombi/sala zetu..
Asante Mungu wetu na tunayaweka haya yote mikononi mwako... Tunakushukuru na kukusifu Daima.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..!
Asanteni sana kwakunisoma/kutembelea hapa.. Mbarikiwe na Ninawapenda.
|