Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 4 February 2015

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi (Pt 1)


Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE

Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi ambaye ametueleza mengi juu ya safari yake kimaisha

Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe. Balozi Nyang'anyi anaelezea

1: Historia yake.

 2: Aliposoma na alivyosoma.

 3: Namna alivyofika / kupata kazi Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC)

 4: Alivyoingia kwenye masuala ya diplomasia na kisha.....alivyoiona nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza 1970. Hii ni safari ndeefu ambayo kwa hakika utapenda kuisikia.

 KARIBU

Sunday 1 February 2015

Muendelee na Jumapili hii Vyema;Burudani Na Dan Em-Halleluyah,Tunakuabudu na...!!!


Wapendwa/Waungwana Muendelee na Jumapili hii vyema,Muwe na Amani,Baraka,Upendo,Tumaini,Hekima na Busara..
Tusifu na Kuabudu..!!!!

1Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Aramu alikuwa mtu mashuhuri aliyependwa sana na bwana wake, kwani kwa njia yake Mwenyezi-Mungu aliiletea nchi ya Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma. 2Katika vita walivyokuwa wakipigana na Israeli, Waaramu walikuwa wamemchukua msichana mmoja mdogo kutoka Israeli, naye akawa anamtumikia mke wa Naamani. 
Neno La Leo 2Wafalme:5:1-27
Naamani aponywa

 3Siku moja akamwambia bibi yake, mke wa Naamani, “Laiti bwana wangu angekwenda na kumwona yule nabii aliyeko Samaria! Angemponya ugonjwa wake.” 4Naamani alipopata habari hizi, akaenda kwa mfalme na kumweleza habari za mtoto huyu. 5Mfalme wa Aramu akamwambia, “Chukua barua hii umpelekee mfalme wa Israeli.”Hivyo Naamani akaondoka, huku amechukua vipande 30,000 vya fedha, vipande 6,000 vya dhahabu na mavazi kumi ya sikukuu. 6Barua yenyewe iliandikwa hivi,
“Barua hii ni ya kumtambulisha kwako ofisa wangu Naamani. Nataka umtibu huu ugonjwa wake.”
7Mfalme wa Israeli aliposoma barua hii alirarua mavazi yake na kusema, “Mbona mfalme wa Aramu anataka nimtibu mtu huyu ukoma wake? Kwani anafikiri mimi ni Mungu aliye na uwezo wa kuua au kufufua? Fahamuni basi, mwone ya kwamba mtu huyu anataka kuniletea mzozo.” 8Elisha, nabii wa Mungu, alipopata habari kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, alituma ujumbe kwa mfalme, akamwuliza, “Mbona umeyararua mavazi yako? Mlete mtu huyo kwangu, ili apate kujua kwamba kuna nabii katika Israeli?” 9Naamani akaenda na farasi wake na gari lake mpaka mlangoni mwa Elisha. 10Elisha akamtuma mtumishi wake amwambie, “Nenda ukaoge mara saba mtoni Yordani, nawe utapona kabisa.” 11Lakini Naamani alikasirika sana, akaenda zake akisema, “Nilidhani kwamba hakika atanijia na kumwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, apitishe mikono yake juu ya mahali ninapougua na kuniponya! 12Isitoshe, je, mito Abana na Farpari ya huko Damasko si bora kuliko mito yote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga humo na kupona?” Akaondoka na kurudi nyumbani, huku amekasirika sana. 13Watumishi wake wakamwendea na kumwambia, “Baba yetu kama nabii angekuambia ufanye jambo fulani gumu, je, hungelifanya? Sasa, aliyokuambia tu ni: ‘Jioshe, ili upone!’” 14Basi, Naamani akateremka mtoni Yordani akajitumbukiza humo mara saba, kama alivyoagizwa na Elisha mtu wa Mungu, naye akapona kabisa. Ngozi yake ikawa imara na yenye afya kama ya mtoto mdogo. 15Ndipo akarudi kwa mtu wa Mungu pamoja na watu wake, akasema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu yeyote ila tu Mungu wa Israeli; kwa hiyo, tafadhali sasa upokee zawadi za mtumishi wako.” 16Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.”Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa. 
Bible Society of Tanzania




"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Sunday 25 January 2015

Msimu wa pili wa Darasa la Kiswahili waanza rasmi DMV


Sehemu ya wanafunzi, wazazi, mwalimu na viongozi wa jumuiya waliohudhuria siku ya kwanza ya darasa la Kiswahili DMV
Awamu ya pili ya Darasa la Kiswahili kwa watoto waishio Washington DC na vitongoji vyake umeanza Jumamosi ya Januari 24, 2015.
Rais wa Jumuiya Bw Iddi Sandaly alipata fursa ya kuzungumza nasi kwa ufupi kuhusu darasa hilo.

Karibu umsikilize



Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu Asha Nyang'anyi. Kushoto kwake ni Katibu wa Jumuiya ya waTanzania hapa DMV Said Mwamende
Baadhi ya wazazi wakiwa nje ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo
Baadhi ya wazazi waliokuwa ndani ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo

Friday 23 January 2015

Mahojiano na JhikoMan kuhusu wimbo wake mpya...Africa Arise


Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania

Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage.

Amezungumza mengi kuuhusu

Karibu usikilize hapa chini



Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja

Monday 19 January 2015

Huyu na Yule...........Mahojiano na Dr na Mama Williams


Karibu kwenye mahojiano ya Dr na Mama Williams.

Waasisi wa AHEAD Inc. Taasisi ambayo iliasisiwa mwaka 1985 na inajishughulisha kubadili maisha ya wengi nchini Tanzania kupitia Elimu, Stadi za Maisha, Afya ya Mama na Mtoto na pia kuzisaidia jamii mbalimbali..

Wamezungumzia mengi kuhusu namna walivyofika Tanzania kwa mara ya kwanza 1974. Kilichowapeleka, walivyoamua kubaki huko mpaka sasa, shughuli za Taasisi yao na mengine mengi

Karibu

Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production

Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com



Sunday 18 January 2015

Muendelee vyema na Jumapili hii;Msipungukiwe na Amani, Upendo;Burudani-MAAGANO,EE BWANA NIMESKIA,MSALABA NITAULINDA,KIU YANGU BWANA BY AIC MAMAJUSI CHOIR


Wapendwa muendelee na juma pili hii vyema,Baraka,Amani,Upendo,Busara na Hekima vitawale..
Mungu azidi kutuongoza katika kunena,kutenda na katika yote..............


22Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu. 23Wanaacha kumwabudu Mungu aishiye milele, na badala yake, wanaabudu sanamu zilizo mfano wa binadamu ambaye hufa, mfano wa wanyama, ndege, au wanyama watambaao.








Neno La Leo;Warumi:1:18-32
Kosa la binadamu
 24Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao. 25Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina. 26Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile. 27Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke, wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu. 28Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya. 29Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya, 30na kusingiziana; ni watu wa kuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye kiburi na majivuno; hodari sana katika kutenda mabaya, na hawawatii wazazi wao; 31hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine. 32Wanajua kwamba sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo hayohayo.

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe sana.