Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 13 July 2014

Tumalizie JumaPili hii na Pastor Donis and Nnunu Nkone- SINGING WITH THEIR CHILDREN

Wapendwa;Natumaini MUNGU anazidi kuwabariki na Mnaendelea Vyema na Jumapili hii..
Iwe Njema,Yenye Heri,Baraka,Neema,Tumaini,Utuwema,Fadhili,Shukrani na Amani.

Neno La Leo;Tumsikilize, Pastor Donis na Familia Yake ......




Shukrani Sana na MUNGU azidi kuwabariki;Donis-andNnunu Nkone

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Friday 11 July 2014

Jikoni Leo;How to Make Mbaazi,Viazi Vya Tamu Vya Nazi na Mswahili Sheikha Agil

Waungwana;"Jikoni Leo"  Mapishi haya yatasaidia sana wanaofunga Mwezi huu[Futari]....
Mengi sina nawatakia Mapishi mema.






Shukrani;Sheikha Agil

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Sunday 6 July 2014

Tuendelee Na JumaPili hii Vyema;Burudani-Furaha Choir London - Tuimbe Wimbo (Muda Tutakwenda Nyumbani)na Nyingine...!!!

Wapendwa; natumaini Jumapili hii inaendelea Vyema,Iwe yenye Amani,Baraka,Furaha,Upendo,Fadhili, Shukran,Utukufu tumrudishie MUNGU.......

Mkimshukuru Baba,aliyewastahilisha kupokea  sehemu ya Urithi wa watakatifu katika nuru.

Neno La Leo;Wakolosai:1:1-29


Nae alituokoa katika nguvu za giza,akatuhamisha na kutuingiza katika uflame wa Mwana wa pendo Lale.




"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima

Saturday 5 July 2014

Mahojiano ya Kwanza Production na Diamond Platnumz baada ya tuzo za BET‏


Diamond Platnumz na DMK kwenye utoaji tuzo za BET Los Angeles
Photo Credits: DMK Global Promotions' facebook page
Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Damond Platnumz. Msanii mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Tanzania
Amejiunga nasi kwa njia ya simu punde baada ya kuhudhuria utoaji tuzo za BET ambako yeye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiwania tuzo hizo.
Kazungumza mengi kuhusu TUZO HIZO.
Alipopokea na alivyopokea uteuzi wake, aliloliona kwenye tuzo hizo, ulinganishaji wake katika utoaji tuzo hizi na za Tanzania / Afika, alichojifunza, faida ya kuja kushiriki hili na hata mikakati yake ijayo kuhakikisha kuwa muziki wa Tanzania unafika mbali zaidi.
SWALI jingine alilojibu ni kuwa....ni kweli kuwa ili muziki wa Tanzania ushinde tuzo ni lazima uwe na mahadhi ya Afrika Magharibi (kama muziki wake wa Number One) ama Afrika Kusini 
Amejiunga nasi kwa msaada wa promota Dickson Mkama almaarufu DMK ambaye pia ndiye meneja wa msanii huyo hapa nchini.
KARIBU





Thursday 3 July 2014

Chaguo La Mswahili Leo;Michelle Williams - Say Yes ft. Beyoncé, Kelly Rowland.!!!!!

Waungwana Chaguo La Mswahili Leo.Say Yes.....
Mmmhhh Maneno mengi sina..Twende sote sasaaaaa.....
.



Mimi umenishikaaa..wewe je?

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana
.

Wednesday 2 July 2014

Mahojiano na Kwanza Production na NURU THE LIGHT‏


Photo Credits: Bongo Celebrity 
Karibu katika mahojiano kamini kati ya Kwanza Production na NURU THE LIGHT.
Msanii, Mjasiriamali, Mtangazaji, Blogger na Mwanaharakati ambaye amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi moja kwa moja kutoka Stockholm Sweden
Kazungumza mengi ikiwa ni pamoja na alivyoanza muziki
Kisha akagusia kuhusu onyesho lake la kwanza kabisa jukwaani.
Na kama nilivyokuja kumtambua, ni mtu mwenye misimamo na anayejitambua, utamsikia msimamo wake awapo studio
Nikataka kujua pia, nini anaona kama tatizo kubwa kwenye muziki wetu?
Haya ni machache kati ya mengi aliyozungumza nami
JIUNGE NASI



Sunday 29 June 2014

Tumalize JumaPili hii Kwa Amani Na Shukrani;Burudani,Solomon Mukubwa - Mungu Mwenye Nguvu,Ni Kwa Neema Na Rehema - Edson Mwasabwite. Na Siku Kama Ya Leo,Kaka Lusungu Ndondole Alizaliwa!!!

Wapendwa,Tumalizie/Tuendelee na JumaPili Hii kwa,Amani Shukrani,Furaha,Upendo na Matumaini.....
Basi, tuseme nini juu ya hayo?MUNGU akiwa upande wetu,ni nani aliye juu yetu?

Neno La Leo;Warumi:8:31-39
Wala yaliyo juu,Wala yaliyo chini,Wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika Kristo YESU BWANA wetu.

Siku Kama Ya Leo;Bibi Na Bwana I.Ndondole Walipata Mtoto wa Kiume.
Hongera Sana kwa Kutimiza Miaka Kadhaa, Mwl. Lusungu Ndondole
MUNGU azidi kukubariki kila iitwapo Leo,Uendelee kuwa Baraka kwa Wazazi,Familia na Jamii pia.
MUNGU akupe Miaka Mingi na Ufanikishe Ndoto zako.


Mhhhhh Ni Kwa Neema Na Rehema.......




"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.