Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 11 August 2013

Natumaini J'Pili inaendelea Vyema;Burudani-Hakuna Mungu kama Wewe na Nyingine!!!!!

Natumaini J'Pili Inaendele Vyema..
Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako,Ee Uliye juu.

Neno La Leo:Zaburi:92:1-5;Ee BWANA jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
Wapendwa/Waungwana; Nawatakia kila lililo Jema, Baraka,Amani na Furaha.






"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Wote.

Saturday 10 August 2013

Watoto Na Malezi; Watoto wa zamani,Mnakumbuka Kipindi cha MAMA na MWANA?



Watoto wa Zamani Mpo? Mnakumbuka  MAMA na MWANA/WATOTO WETU/CHEI CHEIIII..Mhh mimi ni mmoja wa waliokuwa wapenzi  wa Kipindi cha Watoto RTD...
Enzi ya Shangazi/Mama, Debora Mwenda,Sango Kipozi,Eda Sanga na Wengine....

Mhhh Chei Chei Shangaziii..Uje tena Shangazii...


Sehemu ya Kwanza ya Hadithi ya Binti Mfalme;



Sehemu ya Pili



Kujua Mengi Kuhusiana na Watoto Nifuate Huku;http://Watotonajamii.blogspot.com Huku Utakutana na Mambo ya Watoto,Wazazi/Walezi.Hapa tutaendeleza Watoto Na Malezi kwani Swahili Na Waswahili ni Mama Leo..Lakini nimetenganisha Mambo Kidoogo..huko ndiyo Penyewe kwa Mambo ya Watoto na Jamii.

Pia kwa Mambo ya Mitindo Nifuate Huku;http://www.mitindoafrica-abroad.blogspot... Kwa Undani Zaidi..
Panapo Majaaliwa/Kwa Mapenzi ya MUNGU ipo siku yote yatakuwa kwenye Nyumba moja.
Yote Haya yapo Ndani ya SWAHILI NA WASWAHILI NA WAPENDAO YA WASWAHILI NA YASIYO YA WASWAHILI YANAYO FAA KUJUZWA WASWAHILI. 

Pamoja Daima.

Friday 9 August 2013

Tamasha kubwa la muziki wa Injili kufanyika Washington DC kesho!!!!


 Waimbaji wanaofanya vema kwenye muziki wa Injili Afrika Mashariki, Upendo Kilahiro na Christina Shusho, watatumbuiza katika Tamasha kubwa la Injili litakalofanyika Jumamosi hii jijini Washington DC

 Kama walivyoongea kwenye VIDEO HII, waimbaji hao wamekamilisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo pia litashirikisha waimbaji wenyeji wa hapa Marekani.
 

 Tamasha hilo kubwa lililo sehemu ya Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries litafanyika siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi kamili mpaka saa tatu usiku (6:00pm - 9:00pm) na kiingilio kwenye tamasha hilo kitakuwa ni dola kumi ($10) kwa watu wazima, bure kwa watoto.

 Anwani ambapo litapofanyika tamasha hilo ni

 The Way of the Cross Gospel Ministries 

 (at University United Methodist Church) 

 3621 Campus Drive 

 College Park, MD 20740 

 Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na

 Mch. Ferdnand Shideko +1 240 476 6718 ama

 Ms Flora Mnkande +1 240 217 6335

 Waimbaji hawa wote watatumbuiza nyimbo zao za zamani na mpya na wanawaalika watu wote kujumuika nao na waimbaji wenyeji kuweza kupata BARAKA kwa njia hii ya uimbaji

   

   
Zaidi utayapata; http://www.changamotoyetu.blogspot.com
 http://www.youtube.com/user/mutwiba

Mkono Wa EID [Eid Mubarak] Kwa Watu Wote!!!!


Nawatakia/Nawapa Mkono Wa EID [EID MUBARAK]
  Ndugu,Jamaa,Marafiki,Wa Tanzania na Watu Wote Duniani.
Muwe na Eid/Siku Kuu Njema,Yenye Amani,Upendo,Umoja,Baraka na Furaha.



Pata Burudani taratiiibu!!!!



"Swahili Na Waswahili" EID MUBARAK

Zawadi ya shilingi Milioni 10 kwa taarifa za washukiwa Zanzibar!!!!!


Kristie Trup na Katie Gee

Polisi nchini Zanzibar wameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tanzania kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa watu waliowashambulia wasichana wawili waingereza kwa Tindikali.
Wasichana hao kutoka London, Kirstie Trup na Katie Gee, walirushiwa Tindikali kwenye nyuso zao walipokuwa wanatembea mjini Jumatano Jioni.
Taarifa zinazohusiana
afya
Serikali ya Zianzibar ndio itakayotoa zawadi hiyo.
Polisi wanasema kuwa hizo ni pesa nyingi sana kisiwani Zanzibar.
Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania baada ya kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.
Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.
Mama za wasichana hao, Rochelle Trup na Nicky Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo sababu yake haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote. Walishambuliwa na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
Polisi walisema kuwa walirushiwa Acid kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.
Mama za wasichana hao walisema kwenye taarifa yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi kwa nini wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa nia njema.
''Tunashukuru kwa wale wanaotaka kujua kinachoendelea lakini tungeomba vyombo vya habari vituwache kwa sasa hadi tutakapokutana na watoto wetu,'' alisema msemaji wa familia za wasichana hao.
Wasichana hao walikuwa wamekaa Zanzibar kwa muda wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki tatu, kupitia kwa kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema inafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.
Kari Korhonen, mkurugenzi mwenza wa kampuni ambayo wasichana hao walikuwa wanafanyia kazi, alisema kuwa hali yao si mbaya ikizingatiwa athari za Acid kwa mwili na visa ambavyo vimewahi kushuhudiwa vya kuchomwa kwa Tindikali
Msemaji mwingine aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa njiani kuelekea kwa maankuli ya jioni wakati wa shambulizi hilo.

Habari zaidi;http://www.bbc.co.uk/swahili/

Thursday 8 August 2013

Shusho, Kilahiro kuhudumu Washington DC wiki hii!!!!!



 Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).

 Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za  Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.

 Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili

 Maadhimisho haya yatafanyika
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740


 Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.

  Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo



Mengi utayapata; http://www.changamotoyetu.blogspot.com
 http://www.youtube.com/user/mutwiba