Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 16 April 2013

Yanayo endelea Facebook;Mwalimu Ndondole na Wengine...Jee Wewe Unasemaje?


NAMHOFIA MWANANGU... NAIHOFUA KAZI YANGU... NALIHOFIA TAIFA LANGU...... HASA PALE MBUNGE NA WAZILI WANAPOONA BANGI INAWEZA KUWA HALALI KULIMWA (MAANA YAKE NA MATUMIZI YAKE)

HIVI TANZANIA IMEKOSA VITEGAUCHUMI NA RASLIMALI KIASI CHA KUIFIKILI BANGI KAMA ZAO LA KUONGEZA KIPATO....?

MADHARA YA BANGI YANAPOFANANISHWA NA YALE YA SIGARA KUNA UELEWA HAPO?
HAWA NDIO VIONGOZI WETU WANAOFIKIRI KWA KINA KWA NIABA YETU...?

WANAJUA KWANINI WATU WANAFIKIA HATUA YA KUVUTA BHANGI.....?

BINAFSI NAOGOPA...........................................................?

  • Edgar Joel Naunga mkono hoja tunapoteza mapato mengi sana wakati watu wengi wanatumia na ina soko kubwa sana tungepata mapato mengi endapo ingetozwa kodi .
  • Leon Mhongole uwezo wa kufikiri wa wabunge wetu umeshuka sana inatishia maisha ya vizazi vijavyo..
  • Lusungu Ndondole Natamani watoto wa yule mbunge, waziri na Edgar Joel wawe wa kwanza kuanza kutumia hii kitu. Lakini nawaswas na UZALENDO WAO na KAMA WANA WATOTO........ Najiridhisha kwa KAZI ZAO haziwapi fursa ya KUTAFAKARI zaidi ya KUFIKIRI....
  • Lusungu Ndondole Bwana Leon Mhongole, sie wenye WATOTO, UZALENDO na IMANI............ ndio TUNAOTAFAKARI mpaka kufikia tulikofikia. Usiogope ni KAZI zao na MAKUZI yao yanawapotosha...
  • Edgar Joel Mi nilimwelewa sana Mbunge Lusungu Ndondole unajua tumbaku ina madhara makubwa sana na ni sumu lakini imeruhusiwa kwanini bangi nayo isiruhusiwe tafakari na jua kuwa inatumika sana sasa na watu wa rika lote sasa jiulize je tumepoteza vipi mapato..
  • Edwin Mvanda Nadhani watawala washalichoka taifa hili. Wanataka baadae tuwe na taifa lenye vichaa watupu.
  • Kukaye Moto hiyo ndio dawa ya vifua vikuu hamkujua nini hahahaahaha hapa ulaya inauzwa bei sana, karibu nchi zote zimeruhusu ..watu wananunua hapa madukani..Usiogope..acha watu wapate ajila zao kama zao lina kubali ..hiyo sio hatari kama kodi itakusanywa vizuri..Rushwa ni hatari kupita kajani hako
    16 hours ago · Edited · Like · 1
  • Jane Mkini Acha mbwembwe wewe mbona tumbaku inalimwa akat mshaambiwa ni hatari kwa afya zenu!!!!!!!!! Acha tu iruhusiwe hiyo bange ili kama kutatokea nginjanginja basi wajingawajinga wote tufe wabaki wenye akili zao labda kutajengwa taifa lenye usawa na haki.......
    7 hours ago · Like · 1
  • Lusungu Ndondole Dada Jane Mkini Hujaisoma POST sawasawa, kwa uwezo wako wa kutafakari watakaokufa ni wajinga au wavutabangi? Ndio maana nimeuliza UNAFANANISHA MADHARA YA BANGE NA YALE YA SIGARA? Fikiri tena na UTAFAKARI.
  • Lusungu Ndondole Shemeji yangu Kukaye Moto, najua we ni ADIKT WA UZUNGU ndio maana sishangai mchango wako.
  • Lusungu Ndondole Nina maswali muhimu kwa Kukaye Moto, UNAFANANISHA ULAYA NA TANZANIA? We umetokea pale Ipogoro, najua fika unaijua TZ vizuri, UNADIRIKI KUITAFAKARI TANZANIA KWA KUILINGANISHA NA UINGEREZA AU UJERUMANI? Vijana wa kitanzania wapo sawa KIELIMU, KIPATO, UTA...See More
  • Edwin Mvanda Watu hawajui, unapokua na vichaa na mateja wengi ndipo hata wewe uliye na kazi yako unakua katika risk zaidi. Vibaka wakizidi utapolwa na wala hutakua salama. Kwa sasa wafanyakazi wote wanalipa kodi pamoja na ya wote wasio na kazi. Yaani wewe uliyeajil...See More
    15 minutes ago · Like · 1
  • Lusungu Ndondole Kwa maswali yangu hayo kama UNAWATAKIA MEMA wanyalukolo wenzio huku utafikiri UPYA na KUTAFAKARI shemeji yangu Kukaye Moto. Huo UZUNGU ndio ULIOWAHARIBU hata viongozi wetu wakienda ulaya wanarudi wanafikiri na KUWAZA KIULAYA wakidhani watu wote wa TZ wameshafikia kiwango cha
  • Edwin Mvanda Ubinafsi utatuua. Huyu anayetetea bangi ananikumbusha hasira za popo anapokua mtini kalala. Popo anaposikia kishindo cha kitu kinapita chini hupatwa na hasira na hatua ambayo huchukua ni kutoa kinyesi ili kimfikie aliye chini ambaye anahisi ni adui yake, sasa anasahau kua kalala miguu juu kichwa chini ndipo hapo mwili mzima huloa mavi yake mwenyewe. Hivi ndivo tunataka kufanya tunapotetea bangi. Watch out guys.
  • Lusungu Ndondole Sawa kabisa kaka Edwin Mvanda. Tatizo la kuathiriwa na UZUNGU ndilo linalowatesa hata viongozi wetu wengi wakienda semina ULAYA na AMERIKA wakirudi WANAFIKIRI KIZUNGU na KUWAZA KIZUNGU ndio maana wanalopoka tuu wakidhani wote wamefikia MAENDELEO, MAHITAJI, MTAZAMO na MALENGO ya KIMAREKANI wamesahau kama wao wanawaongoza WAFRIKA ambao wengi bado HAWAJAFIKIA KIWANGO WANACHOWAFIKIRIA badala yake walitakiwa WATAFAKARI kwanza.

Like ·              Maoni/Ushauri,Nyongeza......
 Karibuni Sana na Tuelimishane Kwa Upendo.
                                                      "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
 · 

Sunday 14 April 2013

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-Mke mwema!!!!!




Wapendwa muwe na J'Pili Njema na Amani,Upendo,Fadhili,Shukrani,Baraka,Furaha...

Naye alipowaona makutano,alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi,Wanafunzi wake walimjia;

Neno La Leo Mathayo Mtakatifu:5:1-12.Heri masikini wa roho;Maana ufalme  wa Mbingunini wao.Endele.....


"Swahili NA Waswahili" Amani na Upendo.

Siku kama Ya Leo Da'Phoibe Alizaliwa!!!!!




Waungwana Siku kama ya Leo dada yetu Kipenzi PHOIBE Alizawali.

Ujumbe wake hapo chini;

AHSANTE SANA MWENYEZI MUNGU KWAKUNIPA UHAI HADI SIKU YA LEO. SIO KAMA MIMI NI MWEMA SANA ILA UNAMAKUSUDI YAKO YA KUNIWEKA HAI HADI SIKU YA LEO. NAKUSHUKURU SANA MUNGU WANGU, MAMA YANGU WEWE NDIYE ULIYENILETA DUNIANI TAREHE KAMA YA LEO MIAKA 43 ILIYOPITA, NAKUSHUKURU SANA MAMANGU MPNZI NAKUTAKIA MAISHA MAREFU SANA. KWAKO WEWE BABANGU KIPENZI JP NAKUSHUKURU SANA KWAKUNILETA DUNIANI INGAWA SIKU YA LEO HAUPO NAMI. NAKUOMBEA SANA BABANGU NAKUMISS SANA. R.I.P MY DAD. AHSANTE SANA MUNGU KWA MEMA YOTE UNITENDEAYO.


Nasi tunakutakia kila lililojema,Baraka,Amani,Furaha na Maisha marefu kama bibi Mwanapenza......

         "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Saturday 13 April 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Joto Hasira - Lady Jay Dee ft Proffesor Jay New na Nyingine Nyingii!!!!!!!

Mhhh ...hili Joto Hasira..Upepo hakuna....Naruka Mwenyee..nasioni maana ya sisi kuzinguana..kila mtu anajua sana..

Mhhh sikiliza mwenyeweee...Muungwana

Usiusemee Moyo wa Mwenziwako ooohhh.
Mmhh pole  kwa Wanawake wote wanaopitia haya.....
Mhhh...Wameanza tenaaa  oohhh ...Hadithhhh  hadithiiii njoo utamu koleaaa..wanok..nok..
Njoo tu dance njoo dance...

Mhhh......jay Dee mwisho...mmhhh..
Machoni kama watu Moyoni...hawana Utu.Imani imetoweka mabaya yanaongezekaaa..
Mhhhhh..usimpe nafasi.......

Endelea kuburudika na kwenye nyimbo kuna mengi ya kujifunza pia..
Huyu dada mimi huwa ananikosha/napenda sana Nyimbo zake na hata baadhi alizoshiriki..
Huwa sizichoki hata za zamani..nikipata muda nazipitia za Zamaniiiii...
Vipi wewe Muungwana JIDE Anakubamba/kupenda?Katika hizi za Leo ipi imekugusa?

Endelea kuburudika.......

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima

Friday 12 April 2013

Wanawake na mitindo;Lazima uwe Shoshoo Classy!!



Waungwana; Mjumbe hauawi..Mambo ya Urembo..kunamsemo unasema Ukitaka UZURI lazima UZURIKE....
[Hata kama Mzee usiitishe  ule Uzee  lazima uvae vizuri ukawe poa ukawe SHOSHOO CLASSY]!!!!!

 Hahahahaha..Unalo la kuongezea?
 kujua zaidi Mambo ya Mitindo na Urembo Ingia;http://mitindoafrica.blogspot.co.uk/

Shukrani;NTVKenya

                        "Swahiii Na Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 10 April 2013

Unahitaji Logo[Nembo]? Wasiliana na 99graphix!!!!!!






Ili uweze kufikia malengo yako ya kibiashara, unaweza kuwasiliana na 99graphix wabunifu wa aina mbali mbali za logo (Nembo). 99Graphix Design Email: 99graphix@gmail.com http://99graphixdesign.blogspot.com/


au unaweza kuwasiliana nami kwa;Email;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili na Waswahili"Pamoja Sana.