Saturday 5 January 2013
Thursday 3 January 2013
Afya na Jamii;na Mswahili John Haule-Refusha maisha kwa MAJI!!!!!!!!
Refusha maisha kwa MAJI
Hivi karibuni kumetokea uhaba mkubwa wa maji
duniani. Kwa wale tuliozaliwa miaka ya sabini na kurudi nyuma tulishuhudia
watoto wakiogelea katika mabwawa yaliyokuwa yamezagaa nchi nzima, mito ilikuwa
imejaa mpaka watoto walikuwa wakizama na kufa maji, mabomba yalikuwa yakitoa
maji safi na yenye uhakika kila nyumba kwa vile huko yalikokuwa yakitoka
kulikuwa kuna chemchem zenye uhakika wa kutoa neema ya maji safi pia kwa wakazi
wa vijijini.
Maji yanauzwa:
Nyumba za vijijini kama kawaida zilikuwa na
mitungi mikubwa ya kuwekea maji na juu yake kuliwekwa kata ya kuchotea na kunywea maji hayo ambayo yalikuwa na harufu
na ladha nzuri ya ajabu isiyoelezeka labda msomaji wangu unisaidie kuielezea.
Lakini maji hayo pia yalipatikana kwa gharama ya kupiga hodi, kusalimia na
kuomba maji ya kunywa tosha! Vivyo hivyo mijini nako mambo yalikuwa si haba,
hakika iliwezekana pia kupiga hodi nyumba yoyote ukasalimia vizuri na kuomba
maji ya kunywa na wakakuletea galoni la maji lenye umande toka katika friji
pamoja na glasi
ujisevie...
Lakini mambo leo hii yamebadilika. Ndiyo, maji
yanauzwa! Si kiyama hiki jamani? Kiyama kwa maana maji ndio uhai wa binadamu
sasa uhai unauzwa shilingi ngapi? Yanauzwa! kwenye chupa haya, kwenye mifuko ya
plastiki ambayo bila adabu yamepewa jina "maji ya viroba" haya, ya
kupimiana kwenye glasi tuambukizane maradhi haya. Yanauzwa...
Maji ya chupa:
Lakini, hebu tuyaangalie kwanza maji haya
yanayoitwa ya chupa jinsi yanavyopewa urasmi katika matumizi kwa mipango ya
"lifestyle..." Hapana, japo ninaweza nikagusa maslahi ya
watengenezaji wa maji ya chupa nchini kwa hili nitawaomba waniwie radhi maana
wanywaji ni sisi raia tusiojua kitu na kuwapa wao maisha yetu kirehani-rehani
tu. Tabia imejengeka tena ya kukereketa kabisa rohoni kuona watu eti wananunua
lundo la maji ya chupa na kuyaweka majumbani familia ipate maji ya kisasa
zaidi. Wengine ndio imekuwa kawaida kuzunguka na maji hayo kutishia wenzao kuwa
wao hunywa kilicho bora, mambo yao safi.
Maji yaliyofungiwa kitaalamu ni maji maiti.
Maji maiti kwa maana maji ni kitiririka na hupoteza maana halisi au hufa mara
tu yanapokatazwa kutiririka. Hii inajulikana dunia nzima. Kwa kutambua hilo
ndio maana maji yaliyofungiwa huwa yanaharibika yakikaa muda fulani (Expire
date) hii inahitaji macho tu kuisoma katika chupa ya maji yoyote. Hivyo kwa
kuwa maji yakifungiwa hufa, ndio maana unashauriwa kuyarudishia uhai kiujanja
kwa kuyaweka katika ubaridi kabla ya kuyanywa. Na kwa kuhakikisha hilo hebu
kunywa maji ya chupa ya moto uisikie ladha yake ilivyokufa. Hapa sisemi kuwa
maji ya chupa hayafai, ila najaribu kukufahamisha msomaji wangu kuwa maji ya
chupa si rasmi kwa matumizi bali ni msaada tu pale maji rasmi yanapokosekana.
Wewe unatakiwa unywe maji hai tena ikibidi ukinge mdomo katika chemchem....
Maji ya Madimbwi:
Binadamu akishikwa na pilika za kiu huwezi
kumzuia. Akina mama watakuwa mashahidi wangu wazuri maana kesi za watoto kunywa
mafuta ya taa wakidhani ni maji wameshazizoea. Eneo fulani wanaweza wakawa na
shida ya maji salama. Hawa wanaweza kuwa wana madimbwi na mifereji ya maji
lakini wanayaogopa kuyanywa kwa kuwa yameshawapeleka ahera wengi na wengi wao
pale wameshalazwa kwa kuambukizwa maradhi na vimelea vya maradhi vilivyomo mle.
Niliposhiriki "Route Match" na jeshi
fulani hapa duniani nakumbuka nilifundishwa kuweka "Iodine pellets"
ndani ya mkoba wangu kama kinga ya kunywa maji yoyote mbele yangu kwa kuwa
tulitembea siku nane usiku na mchana ndio kikaeleweka. Iodine pellets kwa
kiswahili ni "shabu" tena zipo tele masokoni na pengine madukani.
hutataabika kuzipata na kama itakusumbua nitafute nikusaidie. Chukua punje moja
tu yenye ukubwa wa kunde, tia katika glasi yako yenye maji, acha ikae kwa
dakika tano hadi kumi kisha kunywa maji hayo. Utakuwa salama salimini.
Lakini angalia kuwa kunywa maji ya aina hii
kunataka upelelezi mdogo kwa kutumia akili ya kawaida kabisa. Inakubidi kwanza
kabisa kabla hujafanya chochote chunguza vyanzo vya dimbwi ua mfereji huo kama
unatoka kwenye viwanda au makazi ya binadamu? Siri yako msomaji wangu, viwanda
na binadamu ni wazalishaji wakubwa wa sumu zisizojulikana hivyo ukigundua vyanzo
ni hivyo USINYWE maji hayo.
Maji yenye chumvi:
Kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam hasa
maeneo ya Mbagala wanayajua sana maji haya. Wao wanayapata toka katika visima
vilivyozagaa maeneo hayo maana ndivyo vyanzo vyao vikubwa vya maji wanayotumia.
Maji chumvi kitaalamu si maji salama japo unaweza ukayapata yakiwa safi.
Usalama wake si wa kuaminika kwa kuwa ardhi ina utajiri wa madini ya aina
nyingi zenye tija kwa binadamu lakini ardhi inabeba pia madini yenye sumu
baridi (slow killer agents) ambayo unaweza kuyaonja katika maji na kusema ni
"chumvi" bila kujua ni chumvi gani, na kama ni sumu au la.
Kisima kinachotoa maji yenye sumu baridi za
aina hii hudhoofisha afya za wakazi wanaolizunguka eneo hilo kila wanapoyatumia
maji hayo na siku moja sumu ikiwakolea ndipo mnakutana hospitali wakazi wa mtaa
mzima bila kumjua mchawi wenu na huku dakitari akijikuta haujui ugonjwa wenu
pia... Mtajikuta mmefanana na wakazi wa mji fulani waliokula nyama toka bucha
moja ambalo bila kujua muuza bucha alikuwa anakatia nyama katika gogo la mti
wenye asili ya sumu baridi. Ugonjwa wa ajabu mtaa mzima! Walijikuta mtaa mzima
wamejaa hospitali, hawajulikani wanaumwa nini..... Tutaizungumza mungu
akipenda.
Lakini msomaji wangu siwezi kukuacha yakukute.
Unajua kuitenganisha chumvi na maji ya kunywa ni shughuli kubwa, yenye mipango
mingi pengine kufungua kiwanda. Hapa ninayo mbinu ya kijeshi na ya kisayansi
zaidi unayoweza kujichujia chumvi hiyo na ukapata maji japo kidogo ya kunywa.
Fanya hivi: Chukua beseni tia maji hayo haramu yenye chumvi nenda kaweke juani.
Chukua jagi au kikombe kizito kisichoelea weka
katikati ya beseni lako lakini angalia maji yasizidi yakaingia kwenye chombo
chako na uhakikis ` he chombo hicho hakielei kimetuama kabisa. Chukua karatasi
la nailoni ziba juu ya beseni lako kisha funga na kamba ikaze beseni lizibe
kabisa. Chukua jiwe dogo saizi ya ndimu weka katikati ya karatasi pale juu ili
lilete kauzito fulani.Pamoja na kauzito hako angalia karatasi lisikiguse chombo
ulichoweka ndani.
Subiri maji yajichuje, baada ya masaa matatu
nenda kafunue karatasi. Utakuta maji yenye chumvi ndani ya beseni yamekuwa ya
moto yanatoa mvuke ambao unatengeneza umande kwenye karatasi la nailoni kwa
ndani. Sasa, kwa kuwa nje umeweka jiwe katikati, basi umande ule pale ndani utatiririka
kuja kati kwenye uzito na kisha ni kuangukia kwenye chombo kitupu ulichokitega
kwa ndani. Utakapofungua lile karatasi utakuta chombo chako kina maji na
ukiyanywa ni bariiidi kabisa hayana chumvi. Unaweza ukatengeneza chombo kikubwa
zaidi kama matumizi yako ni makubwa ila utatakiwa kujua namna ya kupiga hesabu
za kifundi. Ukishindwa niite nikusaidie.
Maji ni nini?
Maji ni neema ya kiuumbaji tuliyopewa na mola
wetu bure! Shika hilo maana ukituuliza wanasayansi tutakuambia maji ni molekule
yenye atomi mbili za haidrojeni na atomi moja ya oxygen. Molekule hizo ndizo
zinazounda kitu kiitwacho maji. Hakuna kitu muhimu duniani kama kunywa maji.
Lakini kunywa maji safi na salama ndio busara ya kawaida kwa kila mtu. Maji
hupatikana toka katika chemchem, mvua na vyanzo vingine vingi tu kama vile maji
madini ya visima virefu nk. Umuhimu wa maji kwa binadamu ni mkubwa kupita
maelezo kiasi kwamba wataalamu wa afya wa aina zote duniani wamekiri kuwa maji
ndio uhai. Unaweza ukanywa, ukaoga, ukapikia, ukaoshea, ukanyweshea n.k. lakini
usisahau shughuli za kiroho kama kubatiza, kusilimisha, kutibu, kuapisha na
hata ukija kwangu nitakutibu kwa maji tu! ndiyo, nina ibada ya kuomba chochote
kiwe mwilini mwako kwa maji na ukapona.
Kwanini unywe maji?
Kuna tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa mtu
aliyekunywa lita mbili za maji au glasi nane tu kwa siku alitupa dawa za
maumivu ya viungo baada ya wiki mbili tu. Mwingine alitupa dawa za kizunguzungu
na kuumwa kichwa. Wapo pia walioi
pona bila kujijua maradhi ya aina nyingi sana.
Hebu tujiulize maji huwa yanaenda wapi mwilini?
Kwa ujumla binadamu yeyote ni maji kwa 55%
hadi 78% kulingana na ukubwa wa umbo lako. Labda nikuambie kuwa maji ni
theluthi mbili ya mwili wa binadamu yeyote yule aliye hai hivyo ndio maana watu
wakiamua kukuua hukuchinja. wanakata mshipa mkubwa ubebao maji yote ya mwili
pale shingoni na ukikauka maji umetuaga!
75% ya misuli ya binadamu ni maji
. Mtu asiyekunywa maji hana nguvu, amini
kabisa. kama vipi jiulize mbona mtu akiwa mgonjwa taabani huomba maji na si kinginecho.
Umewaona wauguzi wajanja? Kabla ya yote mgonjwa anapewa dripu za maji kwanza.
Shangaa...
90% ya ubongo wa binadamu ni maji.
Maji katika ubongo humfanya mtu awe na uwanja
mpana mno kifikra katika kufikiri, kutoa maamuzi, kukiri, kusamehe, kushauri na
kila kitu kiitwacho fikra sahihi. Alama ya kwanza kwa mtu asiyekunywa maji ni
ubishi. Ukiona mtu anakuwa mbishi bila msingi basi mthibitishe kwa kumwangalia
sura yake utagundua ni mzee kuliko umri wake... Maji. Ukimsogelea usoni mdomo
wake unanuka vyakula vimevunda tumboni, huyo hanywi maji. Jichunguze msomaji
wangu. Wewe si kikwazo kwa ubishi kwa wenzio? Kama vipi, kunywa maji.
22% ya mifupa ya binadamu ni maji.
Wazee mliofikia umri wa miaka 50 na kuendelea
hebu nawaomba msogee mbele huku. Hapa nawaomba mnisikilize maana nyinyi ndio
walalamishi mno wa maradhi ya mifupa lakini kunywa maji hamjui kuwa ni dawa.
Ukinywa glasi 8 za maji kila siku kwa wiki mbili tu utanipigia simu kuwa
maumivu yameanza kupungua. na ukiendelea kunywa maji kwa miezi mitatu utakuwa
umepona sio tu mgongo, miguu, nyayo, kiuno, kizunguzungu na mengineyo, bali
hata ujana unarudi! Niamini kabisa uone maajabu.
83% ya damu ya binadamu ni maji.
Hili sina haja sana ya kulijadili tena maana
nimelisema hapo mwanzo na nafikiri hata wewe msomaji wangu tutakubaliana tu
katika hili hata uwe mtoto mdogo. Usipokunywa maji unauakaribia mstari wa
kupungukiwa na damu. Utakaribisha pia maradhi ya moyo kwa vivunde vya
unavyokula bila kuviyeyusha na maji vinakuwa sumu kali mwilini na mwisho
utakufa
Kazi za maji mwilini:
Maji yana kazi nyingi mno mwilini, na hata
hivyo nyingi bado hazijawekwa bayana bado mpaka leo lakini nakupa tu hizi
chache ambazo zinatosha kabisa kukushawishi msomaji wangu kuwa mnywaji mzuri wa
maji. Maji yanasafirisha virutubisho vyote tunavyokula pamoja na hewa ya
oksijeni kwenda sehemu zote za mwili. Maji ndio yanayoirutubisha hewa ya
oksijeni katika mapafu, huku yakiwa bado kama korokorokoni kulinda na
kukarabati seli zote za mwili.
Ukisikia mtu anasema kichwa kinauma mara kwa
mara basi huyo hanywi maji! sio kichwa tu kinachouma pale, hata ngozi ya midomo
inabanduka kwa ukavu, ni mwoga, hajiamini n.k. Maji pia hurekebisha joto la
mwili, na ndio maana wakati wa jua wauza maji baridi ni neema kwao na wakati wa
baridi wauza kahawa nao si haba... Lakini ukinywa maji basi ujue hayataishia
mwilini bali yataenda kuchukua nafasi ya yale yaliyotumika na ndio maana ukiuonja
mkojo una ladha kali lakini maji ulikunywa yakiwa matamu.
Shangaa. Kabla ya maabara duniani kisukari
kilipimwa kwa dokta kuuonja mkojo wa mgonjwa ili aubaini ugonjwa! Upo ushahidi
wa kumtibu mgonjwa wa maleria kwa kumpa maji kwa masaa kadhaa tu na akapona.
Wazee narudia tena, mgongo, kiuno, miguu, usingizi, na shida zote za uzee
kunywa maji glasi nane kila siku kwa wiki mbili uone maajabu! Elewa kuwa,
hakika hakuna kisichotegemea maji toka unywele hata kufika miguuni kwenye
ukucha wako.
Faida za maji mwilini:
Ukinywa maji utajisikia mwepesi maana
yanavunja lehemu na sumu na kuzitolea kwenye mkojo. Ukinywa maji vile vile
utapunguza njaa. Wataalamu wa lishe wanasema maji ni kirekebisho cha hamu ya
kula ambacho unatakiwa unywe kabla ya kula ili usije vimbiwa kwa kula zaidi.
Hivyo utajikuta njaa imepungua. Maji hayo pia ni dawa kwa waliozidiwa na uzito
mwili (overweight) maana yanayeyusha mafuta yaliyozidi na kuyatoa kwa mkojo na
jasho na kukupunguzia uzito kila siku.
Maji ni tiba binafsi (pocket doctor) pale
unapo banwa na mawazo labda umechacha, bosi mkali, biashara imedoda, mwandani
anasumbua kichwa chako n.k. kunywa maji mengi kukupunguzia mzigo huo wa mawazo
na hakika utaukubali mpango huu. Maji humfanya binadamu aonekane kama mmea
ulioota kando ya mto na asiyekunywa huonekana kama mmea uliooteshwa juu ya
kichuguu! Wazee, Hakika ujana unarudi. Akina mama, mtaungua sana na hayo
madawa ya kemikali kwa kutojua tu. Maji yanafanya kazi kushinda krimu au
losheni yoyote ile duniani! Hata mimi natafuta mchumba anayekunywa maji walau
glasi sita kwa siku, na nikimtazama kwa macho ajae katika mizani. Anayetaka
kuamini aanze kunywa glasi nane tu kwa siku halafu baada ya wiki mbili aone
maajabu.
Maji kwa wafanyakazi. Wewe kama ni mfanyakazi
bila kujali ni wa sekta gani, jenga tabia ya kunywa maji glasi moja kila baada
ya saa moja halafu baada ya majuma mawili tu utanipigia ukikiri ulivyonufaika.
Maji yanakufanya uwe mjanja. Kwa kuwa yanamiliki 90% ya ubongo basi mtu
asiyekunywa maji ni rahisi kudanganywa, kutapeliwa, kuzubaa, kutoeleweka
maamuzi yako n.k. Maji kwa kuwa yanajaa mwilini kukupa afya na nguvu, basi
anayekunywa maji si mwoga! Ni mtu anayejiamini na ni mshindi kwa wasiokunywa
maji popote: darasani, kazini, biashara, shambani, michezoni n.k. Lakini
ukinywa maji, huumwi hovyo! Amini msomaji wangu, wakati nakupa simulizi hii
tamu malaika wa heri mbinguni wanapiga vinanda kuisifia nguvu hii kuu ya
uumbaji duniani ambako pia Wataalamu wa afya duniani kote wameshikana mikono
wakiirusha juu na kusema "REFUSHA, FURAHIA MAISHA KWA MAJI"
John Haule ni mpelelezi binafsi (Private
investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya kijamii.
Unaweza kumpigia kwa miadi ya ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua
kibinadamu. Anapatikana Car Painters - Temeke Stereo, Sandawe Street, jirani na
Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Wednesday 2 January 2013
Kitabu Kimojawapo cha Prof.Mbele-Africans and Americans: Embracing Cultural Differences
The book is available at http://www.lulu.com/shop/joseph-mbele/africans-and-americans-embracing-cultur... and other internet sites.
Here is a review on Amazon http://www.amazon.com/Africans-And-Americans-Embracing-Differences/dp/1411623...
"Mbele takes on the arduous task of comparing American and African cultural differences, focusing mostly on Tanzanian culture and customs - and he does this in less than 100 pages. Anyone interested in this topic will find mostly anecdotal comments and observations from someone who has spent time on both continents. In the end Mbele notes that people are different and that we should embrace and accommodate our differences as much as possible. This is a good book with good information to consider if you are traveling to Africa anytime soon or hosting an exchange student from Africa.
Kujua Mengi kuhusu Prof.Mbele ingia;Joseph Mbele na http://hapakwetu.blogspot.co.uk/
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana
Poleni Sana; Familia,Wa-Tanzania na Mashabiki wa Sajuki!!!
"Swahili NA Waswahili" MUNGU awatie Nguvu katika wakati huu Mgumu.
Pamoja Daima.
Jukwaa Jipya la Malumbano ya Hoja;Filosofa Forum!!!!!
Filosofa
Forum Imevutia Wengi
Discussion
forum mpya – Filosofa Forum ni jukwaa jipya la malumbano ya hoja. Tangu
kuanzishwa rasmi siku chache zilizopita kumekuwa na mlolongo wa wapenda hoja
kujiunga na kuchangia hoja mbalimbali.
Malengo
ya timu inayoendesha jukwaa hili ni kuhakikisha inampa kila mtu nafasi ya kutoa
mawazo, kuuliza maswali, kuchangia hoja, n.k, bila kujali jinsia, maumbile,
uwezo, cheo, kabila, itikadi au dini. Jukwaa hili limeundwa kwa kuzingatia
maadili ya mtanzania. Maneno ya matusi yananaswa (detected automatically). Ni
rahisi kujiunga au kuchangia hoja. Huhitaji ujuzi wa kompyuta wa hali ya juu sana kutumia. Karibu
ujiunge uelimike na kuelimisha wengine.
Tuesday 1 January 2013
Afya na Jamii; na MSwahili John Haule-Panda maua yafukuzayo Mbu!
Panda maua yafukuzayo Mbu!
Msimu wa mvua unakuja. Hauji kimya kimya. Ni lazima unakuja na maambukizi makubwa ya malaria yatokanayo na madimbwi yanayozalisha mbu kwa wingi zaidi na mbaya sana mbu jike wa anofelesi huzaliwa wengi pia. Mbu hawa ndio vinara wa kuwaambukiza watu malaria na habari mbaya zaidi nilizonazo mkononi nikuwa wanawake hasa wajawazito ndio waathirika wakuu wa maambukizi ya ugonjwa huu kwa vile huzalisha hewa ya karboni nyingi kuliko wanaume na hivyo kuwavutia mbu hawa ambao wanaambukiza malaria kuwafuata na kuwadunga. Hii ndio siri ya foleni ndefu za akina mama na watoto mahospitalini.
Msimu wa mvua unakuja. Hauji kimya kimya. Ni lazima unakuja na maambukizi makubwa ya malaria yatokanayo na madimbwi yanayozalisha mbu kwa wingi zaidi na mbaya sana mbu jike wa anofelesi huzaliwa wengi pia. Mbu hawa ndio vinara wa kuwaambukiza watu malaria na habari mbaya zaidi nilizonazo mkononi nikuwa wanawake hasa wajawazito ndio waathirika wakuu wa maambukizi ya ugonjwa huu kwa vile huzalisha hewa ya karboni nyingi kuliko wanaume na hivyo kuwavutia mbu hawa ambao wanaambukiza malaria kuwafuata na kuwadunga. Hii ndio siri ya foleni ndefu za akina mama na watoto mahospitalini.
Mbu hawa wapoje?
·
Wana
rangi ya kahawia. Akitua katika mwili wako hutega tumbo lake kubwa juu kwa
nyuzi 45 na kuleta miguu yake ya nyuma kuwa stendi za kubeba uzito wa damu
atakayo kudunga!
·
Huweza
kunusa binadamu alipo toka umbali wa mita 50!
Ni kawaida ya msimu wa mvua kuja na hali ya joto inayowavutia watu wengi kutoka nje na kupunga upepo usiku ambao ndio muda muafaka mbu hao kundunga na kuambukiza watu malaria kwa mujibu wa wataalamu. Rumours Africa tumetafiti namna bora ya kuwafukuza mbu toka katika maeneo yote ya nyumba yako, ofisi, hoteli, shule, hospitali, kiwanda na sehemu zingine za kazi ambazo watu hukaa usiku hasa mabaa yanayokesha ambayo pia ni wazalishaji wakubwa wa wagonjwa wa malaria.
Ni kawaida ya msimu wa mvua kuja na hali ya joto inayowavutia watu wengi kutoka nje na kupunga upepo usiku ambao ndio muda muafaka mbu hao kundunga na kuambukiza watu malaria kwa mujibu wa wataalamu. Rumours Africa tumetafiti namna bora ya kuwafukuza mbu toka katika maeneo yote ya nyumba yako, ofisi, hoteli, shule, hospitali, kiwanda na sehemu zingine za kazi ambazo watu hukaa usiku hasa mabaa yanayokesha ambayo pia ni wazalishaji wakubwa wa wagonjwa wa malaria.
Maua yafukuzayo Mbu?
Njia hiyo kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizotugharimu mno kuokoa maisha ya watanzania ni kupanda maua yenye harufu na rangi zinazofukuza mbu kama vile rosemary, cintronella, mchaichai n.k.
Tulitafiti pia ni jinsi gani watanzania watazipata mbegu hizi za maua kwa urahisi lakini tukagundua kuwa ni sehemu chache sana wanazoishi watu wenye uelewa hasa wazungu ndio hupanda maua haya bila kuwaambia wengine na kuwaacha watanzania wengine wapande maua kama urembo tu badala ya dawa na vyakula, na hivyo kujikuta wakipata wakati mgumu kupambana na malaria.
Kwa sasa bado tunafanya mpango wa kutafuta wadau wa kuwekeza kuanzisha bustani ya maua hayo ili tupate mbegu kusaidia watu lakini kwa mwenye haraka zake kujikinga na malaria ni gharama kidogo maana itabidi kusafiri mpaka Peramiho Mission au Uwemba Mission ambako nimeyaona kwa macho mashamba yanayozalisha maua yakiwemo hayo na kusafirishwa ulaya. Pengine labda niliwahi sikia tu kuwa hata Arusha pia kuna mashamba ya maua pia lakini upatikanaji wake kwa kweli siujui.
Maua haya hatimaye yatasambaa. Kila mtu nahisi angependa kupanda maua yenye maana halisi katika maisha na hasa kumlinda yeye, familia, wafanyakazi na wateja pia. Hivyo yeyote ambaye amevutiwa na habari hii na angependa kushiriki kwa namna yoyote kuwekeza katika fursa hii muhimu na adimu kwa taifa letu basi angewasiliana na rumoursafrica kupitia simu namba 0768215956 au email rumoursafrica@gmail.com.
Ujumbe huu unaweza kuwa muhimu kwako, lakini unaweza kuwa muhimu kwa wengine pia hivyo ningekuomba msomaji wangu uufikishe ujumbe huu kwa wapendwa wako ukisisitiza umuhimu wa kujikinga na malaria.
Asanteni kwa kunisoma.
John Haule ni mpelelezi binafsi (Private investigator)
anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya ushauri juu
ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car Painters - Temeke Stereo, Sandawe Street,
jirani na Dr. Massawe. Simu:
0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
Karate: J.Kassam Ft Juma Jazz!!!!!
mwanamuziki chipukizi lakini mkongwe kwa umri Juma Kassam ,ambaye pamoja na Muziki pia ni muigizaji
na mwanamichezo hususani mchezo wakujihami KARATE.
Usikilizewimbo wake unaojulikana kwa jina la "KARATE" future-ring Juma Jazz na uone jinsi alivyokuja na muelekeo mpya
zaidi ya vile tulivyozoea ya nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana
Subscribe to:
Posts (Atom)