Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 22 December 2012

Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)


 Mfululizo wa 147 Critics ambayo ni  mahojiano ya wadau wa Filamu na Muziki yaliyofanywa na TFCA-
Tanzania Film Critics Association(On line Platform) kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
ambayo yatapelekea kuanzia mwezi wa January 2013 bidhaa zote za Filamu na Muziki zilizopo hapa Tanzania kuwekewa 
Stamp/Sticker kwa ajili ya Kurasimisha,Kumpatia kipato halali msanii na Kukusanya mapato ya serikali yanayotokana na 
uuzaji wa kazi husika.
Sheria hii ina changamoto nyingi ambazo kama hazitatatuliwa zinaweza kuifanya sheria husiaka isfikie malengo yake,Je 
wadau wanasemaje kuhusiana na hilo?

Tusikilize 147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)  akiwa ni mtu wa kwanza kutupa maoni yake kupitia Video hii;


Mahojiano haya yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
98. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
ii. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda
mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na
kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo
hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.
80
Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni
pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali,
utekelezaji wa hatua hii utaanza rasmi tarehe 1 Januari,
2013.

Tunaangalia uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza kuleta ukombozi wa kweli.
           

 Kujua Zaidi Ungana na mwenzangu;TheImageProfession
              
  "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Music Festival 2012:Banana Zorro & B Band!!!!!!



B Band chini ya kiongozi mmiliki Banana Zoro ikitoa burudani ya moja kwa moja kwenye Tamasha kubwa la muziki wa dansi Tanzania lililofanyika kwa siku mbili tarehe 28 na 29 Septembe ,2012 ambalo lilishirikisha bendi mbalimbali maarufu katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
B Band chini ya kiongozi mmiliki Banana Zoro ikitoa burudani ya moja kwa moja kwenye Tamasha kubwa la muziki wa dansi Tanzania lililofanyika kwa siku mbili tarehe 28 na 29 Septembe ,2012 ambalo lilishirikisha bendi mbalimbali maarufu katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
Bendi zilizoshiriki ni DDC Mliman Park 'Sikinde', Msondo Ngoma, B-Band ya Banana Zoro, Mashujaa, Akudo Impact, FM Academia na Wazee Sugu chini ya King Kikii 'Sugu'.

Zaidi usikose kutembelea;TheImageProfession

                 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday 19 December 2012

Mswahili Wetu Leo;SUSU COLLECTION BY SUBIRA WAHURE FOR SWAHILI FASHION WEEK 2012

Dada Subira Mwenyewe ni huyu wa Mbele!!!!


Waungwana;Mswahili wetu leo si Mwingine ni da'SUBIRA WAHURE.
Ni dada Mdogo mwenye mambo Makubwa!!!!!

Hizi ni Baadhi ya Kazi zake.Kujua Mengi kuhusu dada huyu ingia;http://subirawahure.blogspot.co.uk/

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima

Tuesday 18 December 2012

Waswahili Na Maisha Yao;AFRICAN VILLAGE LIFE!!!



Waungwana; Leo tuangalie Maisha ya Kijijini..........

Jee wewe umewahi ishi kijijini?
 Nini kizuri unakumbuka  na Nini kibaya unakumbuka?.....

Jee Unafikiri kwanini Wazungu hupenda kuchukua Matukio ya Vijijini? kwa sababu ni mageni kwao,Wanataka kutusaidi au?.

 MUNGU Ibariki Afrika,MUNGU Ibariki TANZANI!!!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Sunday 16 December 2012

Natumai Mlikuwa na J'Pili Nzuri;Burudani-Bado Sijafika - Kijitonyama Evangelical Choir!!!!

 

Wapendwa;Natumai Mlikuwa na J'Pili Njema.
Kama kuna iliyomwendea Vibaya Pole na Tambua  MUNGU yu pamoja nawe na hajakuacha!!!!!!!!!

Neno la Leo;BWANA ndiye mchungaji wangu,Sitapungukiwa na kitu.ZABURI:23:1-6.

"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Monday 10 December 2012

Da' Mamie Msuya;Anawakaribisha kwenye MISA Ya mama Yake Mpendwa!!!









Mrs 'Mamie Msuya



Familia ya Mr&Mrs Liberty Msuya inapenda kukualika/kuwaalika katika misa ya arobaini ya mama yao mpenzi; BULUNGU. (RIP) .

Itakayofanyika Jumamosi tarehe 15/12/2012,saa 8:oo Mchna[2:00pm]. 
katika ukumbi wa; Henley Green Primary School/Community Centre, Wyken Croft CV2 1hq.
  
Dress code black, white, or purple.
Kwa Mawasiliano Zaidi;07405389488[da'Mamie Msuya]

Ukipata Ujumbe huu wajulishe na wengine.
  Asanteni  na Karibuni Wote.

Sunday 9 December 2012

Nawatakia J'Pili yenye Neema na Baraka;Burudani-Hellen Ken - Peleleza na Nyingene Nyingi!!!!!!

 



Wapendwa; nawatakia J'Pili yenye Neema,Baraka,Amani na Upendo.
Tena ndugu zetu,twawaarifu habari ya Neema ya MUNGU,Waliyopewa makanisa ya Makedonia;

Neno La Leo;2Wakorintho:8:1-15;Maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi,wingi wa furaha yao na umasikini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.

"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Wote.