Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 15 April 2012

Nawatakia J'Pili njema,Burudani-ni wewe baba unaweza na Sifa ni kwako- living water choir!!!!!!!

Muwe na J'Pili Njema woote, Yenye Amani,Furaha, Upendo na Umoja.
Mungu akasema Iwe nuru;Ikawa nuru. Mungu akaiona Nuru,ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
Neno la Leo.Mwanzo1:1-8.
Mbarikiwe sana,Upendo Daima.

Friday 13 April 2012

Chaguo la Mswahili Leo;Swahili Taarab Bi Malika - Sitaki sitaki na Vidonge,Isaa Matona-Msumeno!!

Waungwana Mwajionaje na Khariiii?Teheheheeheh .Nimatumaini yangu woote wazima,Leo nimewaletea Taarab za Zamani kidogo,Hizi Taarab hasa hizi za Zamani zinamafumbo sana, yaani kunamaneno mengine unaweza usiyaelewe anamaanisha nini.
Jee wewe ni mpenzi wa Taarab au huwa unasikiliza/kuangalia au kucheza?
Unaona tofauti gani kati ya Taarab za Zamani na sasa na jee Unafikiri Taarab za Zamani Zinamvuto zaidi ya sasa au Za Sasa Zinamvuto kuliko za Zamani?
Karibuni sana kama hujahi kuzisikia Leo jaribu, na Wapenzi wa Taarab Jimwageni Uwanjani au...Swahili na Waswahili.Pamoja sana tuu!!!!!

Thursday 12 April 2012

Siku kama ya leo da'Victoria-Ruth Alizaliwa!!!!!!

Siku kama ya leo Bibi na Bwana Malonga wa Tanga,Walipata mtoto wa kike na wakamwita Victoria-Ruth.
Hongereni sana wazazi/Walezi na Mungu awabariki sana.


Hongera sana da'Vick-Ruth kwa kuongezeka,Mungu azidi kukubariki na kukulinda siku zote za maisha yako.
Uwe baraka kwa wazazi/walezi ndugu,jamaa ,marafiki  na watu wote wadogo kwa wakubwa.
Uwe na Wakati mzuri leo na siku zote.MUNGU NI PENDO.


Swali la Kizushi:Wapendwa eti watu wenye kutumia the,thatha badala se au sasa,Athante,ASante,walipokuwa watoto walinyonya vidole sana,walideka,walichelewa kuongea au.......


Karibuni Waungwana!!!!!!

Tuesday 10 April 2012

Maelfu ya watanzania wajitokeza kumzika Kanumba Jijini Dar !!..pata na [Video]


Safari ya Mwisho ya Mpendwa wetu Kanumba.Sisi Tulikupenda Lakini Mungu amekupenda zaidi.Ulale kwa Amani.
Picha kwa Masaada wa kaka LUKAZA wa http://josephatlukaza.blogspot.co.uk,Ubarikiwe.
Video kwa msaada wa[ Michuzi blog]http://issamichuzi.blogspot.co.uk.Ahsanteni Sana na   Tulie kwa Amani yeye Amekwenda..

Steven Kanumba (kauli yake ya mwisho) [HD]

Monday 9 April 2012

MAMA KANUMBA KAFIKA DAR NA RATIBA YA MAZISHI KAMA IFUATAVYO!!

 


WAKATI MAOMBOLEZO YA MSIBA YAKIENDELEA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFIKA KUTOA MKONO WAPOLE  AMBAPO LEO MHESHIMIWA PREZIDAR J.K ALIFIKA NYUMBANI KWA KANUMBA KUTOA MKONO WA POLE, NA KESHO ASUBUHU WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA ANATARAJIWA KUFIKA  KUTOA MKONO WA POLE KABLA YA KUELEKEA MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE LINALOANZA JUMANNE
 RATIBA YA MAZISHI IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI.
R.I.P KANUMBA
Habari hii kutoka http://8020fashions.blogspot.co.uk.

Ahsanteni sana.

Saturday 7 April 2012

MAMA KANUMBA AONGEA;Mmmmmhh Pole sana Mama!!!!!!

Mama Mzazi wa Kanumba.
Mmmmhh,Pole sana Mama,Mungu akutie nguvu.
Picha na Video,kutoka ;http://bukobawadau.blogspot.co.uk   Ingia hapo kujua zaidi.Ahsanteni sana.