Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 31 December 2011

YOU CAN HIRE THIS CAR IN DAR ES SALAAM!!!!!






The car with a driver will only cost you 500SEKfor one day in the city of Dar-es-Salaam.
About 60 Euro, 48 pounds, or 75 USD.For trips outside Dar contact us.
Torbjörn Klaesson +46 70 2217044mail: matetereks@gmail.com OR....
Yasinta Ngonyani +46 70 2569176 mail: ruhuwiko@gmail.com

Friday 30 December 2011

MKESHA MKUBWA WA KULIOMBEA TAIFA -ZANZIBAR!!!!!!!!


                       
                                                 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkesha wa Kuliombea Taifa Mchungaji Saimon Mputa katikati akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maandalizi ya Mkesha huo katika ukumbi wa Habari Maelezo Raha Leo,Mjini Zanziba kushoto kwake ni Katibu wa Kamati Mchungaji Edward Mashimba na kuliani kwake ni Mjmbe wa kamati hiyo Askofu Obeid Fabian
                                      
                                                       
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 29/12/2011

Wananchi wa Zanzibar wameombwa kushiriki katika Dua maalum ya
Mkesha wa kuliombea taifa la Zanzibar ilioandaliwa na Umoja wa Makanisa
Zanzibar ambapo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Add
anatarajiwa kuwa Mgeni.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha
huo Mchungaji Simon Mputa alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo uliopo Raha leo Mjini Zanzibar.

Amesema dua hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia majira ya usiku
wa kuamkia Mwaka 2012 katika Uwanja wa Mao tse Tung lengo lake kuu
ni kuliombea taifa kuepukana na majanga mbali mbali ambayo yanaweza
kulikumba Taifa hilo.

Mchungaji Simon amesema sambamba na kuliombea taifa pia kutafanyika
maombi maalum ya shukrani kwa Mungu juu ya kupatikana kwa Serikali ya
Umoja wa kitaifa Zanzibar pamoja na kuwaombea viongozi wake hekima na
busara katika uongozi wao

Aidha ameongeza kuwa kuna haja ya wananchi kukaa kwa pamoja na
kuweza kumuomba Mungu ili kuyaepusha majanga yaliyoikumba Tanzania
mwaka 2011 yasiweze kutokea tena katika Mwaka mpya wa 2012

Ameyataja majanga hayo kuwa ni pamoja na ajali ya kuzama kwa Mv.
Spice Islanders Zanzibar na Mafuriko yaliyoikumba mikoa ambali mbali ya
Tanzania Bara ikiwemo Dar es Salaam na kusababisha vifo vya wananchi
wengi.

Kwa upande wake Katibu wa Mkesha huo Mchungaji Edward Mashimba
amesema maandalizi ya Mkesha huo yamekamilika na kuwataka wananchi
wa Zanzibar kushiriki kwa wingi bila kujali itikadi za dini wala siasa zao.

Mchungaji Saimon amesema Maombi hayo ni maombi shirikishi ambayo
hapo awali yalikuwa yakifanywa na watu wachache lakini kutokana na
mwamko wa watanzania kumesababisha maombi hayo kufanyika katika
viwanja ili kukidhi haja ya wageni wanaoshiriki

Naye Mraribu wa Tamasha hilo hapa Zanzibar Allen Mbaga amesema

Mkesha wa Maombi wa kuliombea Taifa utafanyika katika mikoa mbali
mbali ya Tanzania Bara na Visiwani ambapo washiriki wa Zanziabar
watapata burudani mbali mbali kutoka kwa vikundi vya Kwaya huku
huduma ya za vitafunwa na vinywaji vikiwa vinapatikana Uwanjani hapo.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Ulale kwa Amani Bw,John Ngahyoma!!!!!!

Shirika la utangazaji la habari BBC, limepata pengo kwa kuondokewa na Bw. John Ngahyoma.
Aliefariki dunia leo asubuhi jiji Dar es salaam.


Enzi za uhai wake Bw.John Ngahyoma aliwahi kufanya kazi katika kituo cha habari cha Radio Tanzania Dar es salaam(RTD),ITV Radio One na baadaye TVT.
Mpaka mauti inamfika Bw.Ngahyoma alikuwa anaitumikia BBC.


Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata

Taarifa imetolewa na katibu mkuu jukwaa la wahariri BwNeville Meena.

Thursday 29 December 2011

Mswahili wetu leo ni-LULU MICHAEL,Hapa alikuwa Mwanafunzi!!!!!!

LULU akiongelea maisha yake baada ya MIAKA 18 ndani ya TAKE ONE

Watoto na Vituko-African Dance!!!!!

Ulale kwa Amani da'Halima Mchuka!!!!!

DADA HALIMA WAKATI WA UHAI WAKE.

Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC – HALIMA MCHUKA amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI Jijini DSM alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa kiharusi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA, HALIMA MCHUKA alikimbizwa katika hospitali ya DAR GROUP na baadae katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI hapo jana baada ya kuanguka ghafla akiwa katika kituo chake cha kazi eneo la PUGU ROAD Jijini DSM.
MCHUKA alikuwa mtangazajii wa kwanza wa kike wa mpira AFRIKA MASHARIKI.

               Poleni sana Familia ya Mchuka kwa wakati huu mgumu kwenu.


                                                       R.I.P. DA'HALIMA.