Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 18 October 2011

AIBU GANI HII BADO INAENDELEA KULIKUMBA TAIFA LETU!!




Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang'hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa!
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.
                                                            
                                                                          Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog
                                                             Asante sana kaka Kapinga.

YUSTA MSOKA, MWANASHERIA ALIYEFANIKIWA KUTIMIZA MOJA YA NDOTO ZAKE.




Advocate Yusta Msoka

Yusta Msoka akiwa amesimama nyuma, mbele ya dirisha la pili upande wa kulia, akiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wenzake baada ya kula kiapo cha kuwa Advocate (Wakili)

KAPINGAZ Blog inapenda kumpongeza sana Dada Yusta kwa kufanikiwa kufika hapo alipofikia, vile vile inamshauri asiishie hapo aendelee zaidi mpaka aweze kufikia level ambayo ni ya kimataifa.

Kwa kutambua uhaba mkubwa wa Mawakili katika Taifa letu tunapenda kuwapongeza wale wote walioweza kufanikiwa kuwa Mawakili, tunawaomba wakafanye kazi zao kwa uadilifu na kuliletea sifa na mafanikio mazuri taifa letu, hasa hasa kuwa makini katika mikataba mikubwa ambayo taifa letu sasa linaangamia kutokana na mikataba hiyo.
                                                                             Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog
                                                              Hongera da' Yusta.

SAKATA LA MGOMO WA WANACHUO WA IMTU UNIVERSITY HATMA YAKE LINI?




Geti kuu la kuingia Chuo kikuu cha Afya IMTU kilichopo Mbezi Beach.

Wanachuo hao hapa wakiwa katika moja ya maandamano ya mgomo huo.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa

Sakata hili lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu mgomo huu wa wanachuo hawa.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari, kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.

Kwa kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia na kuongoza  ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya binafsi (private).

Sisi kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania Commision of Universties na Higher Education Student Loan Board tunawaomba waumalize mzozo huu.
Pesa nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili tatizo ili tuweze kuendelea na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa Madaktari.


Habari hii nimetumiwa na Kapingaz Blog.
Asante.

Thursday 13 October 2011

Mazishi ya Mpendwa Wetu; Baba Mzee Juma Penza, katika Picha

                       Marehemu Mzee Penza wakati wa Uhai wake.
     Kaka Mashaka akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Kaka Mustapha akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Kaka Iddy akiweka Mchanga wa Mwisho.
                   Rais Jakaya Kikwete akiweka Mchanga wa Mwisho.
               Mzee Janguo akiweka Mchangawa Mwisho.
             Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa, akiweka Mchanga wa Mwisho.
       Wajukuu nao hawakuwa nyuma kufanikisha Mazishi ya babu yao.


Shukrani kwa Wote Mliofanikisha Mazishi ya Mpendwa baba Yetu Mzee Juma Penza[JP].
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI;AMINA.


Rachel-siwa[Mwanapenza]na Timu Yote ya SwahilinaWaswahili;MAJONZINI.




picha kwa hisani ya Michuzi blog,Asante sana.

Ulale kwa Amani baba Mzee Juma Penza!!!!!!!

Mzee wetu mpendwa Umetutoka tukiwa bado tunakuhitaji.
Leo sina mengi ya kusema;
Mungu akulaze mahali pema peponi Amina.

Poleni ndugu zangu wote mliopo nyumbani Tanzania na Wote tuliopo nje ya Tanzania,
Tuungane pamoja kwa wakati huu Mgumu kwetu Mgumu.

wako Rachel-Siwa[Mwanapenza].