Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 3 April 2011

Mungu Wabariki kina Mama wote !!!!!!!!!!!!!!!




Leo ni siku ya MAMA  Uingereza.Nichukue fulsa hii ya kuwatakia Kheri,Baraka,Mafanikio,Heshima,Upendo,Fadhili.
Mama yangu Mpendwa na Wamama Wote pamoja na mimi mwenyewe.Sijutii kuwa mama na Asante sana Mumewangu Isaac na Wanaume/kina baba Wote. Pasipo    ninyi  tusingeitwa mama.Pia Poleni sana mliopoteza/Kufiwa na mama,Mungu awalaze mahali pema peponi.
Mpendwa kwa kazi hizo na nyingine nyingi kila siku za kina MAMA,Tusiposaidiana na kina BABA,kweli tutapata wakati wa kupumzika?karibuni sana kwa kuelimishana na kutakiana kheri,kupongezana na unaweza kutupa kumbukumbu zako siku ambayo unahisi ulimfurahisha sana mamayako na siku uliyo muudhi sana mama yako!!.Na unapenda kumwambia nini mama yako?.MAMA NI KIUNGO CHA FAMILIA!!!!!!!!!!!

Monday 28 March 2011

Jikoni leo ni kwa Babu Ambi!!!!!!!!!!!!!!!!

Haya wapendwa jikoni kwa babu leo!!vipi wewe binafsi kikombe cha babu Ambilikile unakiamini?.
Sema na Moyo wako!!!!!!Nasi tunataka kujua mawazo yako kuhusu jikoni kwa Babu wa Loliondo!!!!!!Karibuni sana!!.

Friday 25 March 2011

Pozi la leo!!!!

Mpendwa picha na pozi.Unakumbuka picha za zamani za studio imepambwa maua?
Kama si sasa ulipiga ulipokuwa mtoto au wazee/wazazi wako,Je inakukumbusha nini/wapi?.Karibuni sana!!!.

Thursday 24 March 2011

MSIBA KWA FAMILIYA YA MZEE NGONYANI!!!!!!!!!


DADA  ASIFIWE NGONYANI HATUNAE TENA!!.









Mpendwa /Bloga wetu da Yasinta na Familiya ya Ngonyani,Wanasikitika kutangaza kifo cha Binti/dada yao mpendwa ASIFIWE NGONYANI.Kilichotokea tarehe 23/03/2011.Nyumbani Tanzania,kwa maelezo zaidi ingia www.Ruhuwiko.blogspot.com. kwa niaba yangu na familiya yangu na wapenzi/wafuatiliaji wote wa SwahilinaWaswahili, Tunaungana pamoja na Familiya ya Ngonyani katika wakati huu mgumu na kutoa pole zetu kwenu!!!SISI TULIMPENDA LAKINI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI!!!.

Monday 21 March 2011

Wanaume na Mitindo!!!!!!!!!!!

Leo sina la kusema wapendwa!!! Naicha hii mada mikononi mwenu!! Inaweza kuwa nzuri kwako/mbaya kwa mwenzio.Je wewe Mwanamke/dada unapenda Mumeo aweke vipi Nywele zake au atoke vipi?Haya na Wanaume jee ukiwananywele zipi au mtindo gani  unajiona ukobomba?  Karibuni waungwana ,Raha jipe mwenyewe au?.

Wednesday 16 March 2011

Kuna Wanaojikondesha na Wanaokonda si kwa Kupenda!!!!!!!!!!!!!

Wapo  wanaotamani  hata Uji wa chumvi na hawapati,Wapo wanaoweza kupata chakula chochote watakacho,lakini hawali kwa sababu wanafanya Diet. Wapo wafujaji, waharibifu na wachoyo.Wapo wanaopenda kusaidia waliokosa lakini wana vichache.Binadamu tujenge tabia ya kusaidiana / Kutoa ni Moyo si Utajili!!!!! Wewe unamawazo/mchango  gani katika hili? Karibu tuelimishane Wapendwa!!!!

Saturday 12 March 2011

Wanaume Wanaopigwa na Wake zao!!!!!!!!!!!

Hivi  kuna Wanaume  wanaopigwa  na  kunyanyaswa  na  Wake zao? Je nao wanakitengo cha kuwasaidia kama vile Tamwa na kwingine? Kwanini  kelele nyingi/mashitaka mengi  niyasikiayo  ni ya Wanawake,Au Wanaume ni wavumilivu,wanaona aibu,wanajikaza kiume au wao hawaumizwi na wakiumizwa wanayamaliza wenyewe? Karibu tuelimishane wapendwa!!!!!!!!.