Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 12 October 2011

HALI YA MTOTO CESILIA NI MBAYA ARUDI BILA KUFANYIWA OPERESHENI.




Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamalia wema waweze kumsaidia.

Hapa Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.

Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.

Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.

Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa uchunguzi tunaweza tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
Habari hii kutoka Kapingaz Blog

Tuesday 11 October 2011

Da'Tamara-Sibusisiwe Atimiza mwaka 1!!!!!!!!!

                    Da'Tamara kama anaota vile!!!!!!
  Duhhhh sasa nimetimiza mwaka, Hawa wazazi sijui watanipeleka Boarding..?
                            Mwenyewe mama Tamara!!
Baba Tamara [kaka Manyanya] naona  kajibebea Tamara wake.


Hongera da'Tamara kwa siku yako hii Muhimu, Mungu akubariki katika yote.
Baba na Mama Tamara; Hongereni  sana na Mungu awe nanyi daima katika malezi ya da'Tamara
na Maisha yenu.


Zaidi kuhusu Tamara na Wazazi wake na menginemengiiiii!!! Ingia http://ninaewapenda.blogspot.co

Sunday 9 October 2011

Mahojiano na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Christina Shusho!!!




Habari kutoka kwa kaka Mubelwa[MB].Zaidi ingia;http:www.changamotoyetu.blogspot.com

Rick Tingling on 2011 Julius Nyerere Day



Habari hii nimetumiwa na kaka Mubelwa,Bandio[MB].Zaidi ingia, http://www.changamotoyetu.blogspot.com

Wednesday 5 October 2011

KITENDO TULICHOKILAANI KUTENDEWA MKUU WA WILAYA IGUNGA CHAJIRUDIA TENA, NANI WA KULAUMIWA.







Mwanamke mmoja jana aliyesadikiwa ni mwanachama wa CHADEMA alibebwa mzobe mzobe na Askari wa kutuliza ghasia Igunga baada ya kutokea mtafaaruku kati ya wanachama wa CHADEMA na Polisi muda mfupi kabla ya kutangazwa matokeo ya mshindi wa kiti cha Ubunge igunga.

Napenda wadau tuliangalie hili, hasa taasisi zote za kijamii na kiserikali, hivi majuzi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mama Fatuma Kimario alidhalilishwa kwa kuvutwa na kuvuliwa kilemba na wafuasi wa chadema, kitendo ambacho kililaaniwa na taasisi zote za kijinsia, kijamii na kiserikali. Leo hii linatokea tena tukio kama lile, la mama huyu kuzalilishwa kijinsia kwa kushikwa mwili wake bila ridhaa yake, naziomba taasisi zinazohusika na haki zitueleze je huyu mama hii ni haki yake kutendewa kitendo kama hiki au kwa sababu ni kutoka chama cha upinzania au kwa sababu ni mwanamke asie na madaraka yoyote? La hasha! nadhani hapo hiyo siyo haki.

Naamini jeshi la polisi linao askari wa kike, kwa nini hawa wasitumike kuwakamata waandamanaji wa jinsia yao! mpaka askari wa kiume anadiriki kumbeba huyo mama! Je angekuwa ni mama yake angeweza kumbeba hivyo?

Mi kwa mtazamo wangu nadhani kuna haja ya kuundwa taasisi maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya jinsia hawa askari wetu nadhani itaweza kusaidia udhalilishaji huu usiwe unajitokeza.

KAPINGAZ Blog haifungamani na chama chochote cha kisiasa, Tungependa kuwasikia TAMWA, TGNP na Taasisi nyingine za kijinsia  mkikemea na kuvilaani vitendo hivi.  Tulitegemea kitendo kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya kinaweza kikawa funzo pia kwa askari wetu lakini tunaona bado kinarudiwa tena.

            Imetumwa na KAPINGAZ Blog.