Friday, 4 February 2011

Jikoni leo ni Makande!!!!!!!!!!!!


Leo ni mwendo wa Makande wapendwa .Wengine wanayaita Pure sijui wewe  unayaitaje!!!! Jee wewe vipi  unayapenda ?na unapenda kushushia na nini chai,juisi,maziwa,maji au?karibuni !!!!.

23 comments:

  1. mimi huwa nayaita MAKANDI KWA KINGONI na kibena NGANDE yaani wewe dada wee huna hata huruma umeniona nipo hapo mlangoni nifungulie basi au nso unataka nishibe kwa halafu tu? yaani sikimbuki ni lini nimekula ngoja nijitahidi niyapike nami siku moja. Mie huwa nashushia na maji:-)

    ReplyDelete
  2. hahahahhha jamani da Yasinta nimukufungulia mlango dada yangu naona umesha kimbia au huu upepo wa leo umeshindwa kuvumilia?

    wapikie watoto na shemeji natumaini watayapenda,huko kwako mahindi na maharage hakuna?jamani unakosa uhondo dada yangu!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Sie WAPARE hiyo ni PURE! Na hapo kwangu huwa napenda kuwa na maparachichi aka MAAVOKADO pembeni! Na haki ya nani nashangaa walao makande kwa sukari na sio chumvi!

    ReplyDelete
  4. Mmmenikumbusha Afrika hata kama mimi si mpare nile Pure kama asemavyo mtakatifu Kitururu. Good job ya kutushusha mimate bure.

    ReplyDelete
  5. Basi hiyo ndio NYWILA (password) aliyoitumia Mama P kuninyaka.
    Hahahahaaaaaaaaaaaa
    Mama P anavyojua kuyatengeneza hayooo. Yeye HAPIKI, anatengeneza. Hataki kelele ayapikapo (utadhani anacheza Golf tena PGA).
    Kishushio ni kama alivyosema Mtaka"tifu" K. I guess kwa kuwa wote ni walewale kina "thithi"
    Mimi umenikumbusha JUZI tu, maana ndio niliyala hayo
    Swaaaaaaaaaaaaaaafi

    ReplyDelete
  6. shughuli ya makande ilikuwa lini? Yamekolea nazi hayo! Mimi naona yanapendeza sana ukinywa na chai. Wengine wanayaita kidheri

    ReplyDelete
  7. Kikwetu tunayaita MASANGU...upo hapo?

    Hata hapa huwa nayapika mara moja moja.

    ReplyDelete
  8. duh umnikumbusha mbali sana na wala sikumbuki ni lini mara ya mwisho kula ila nitahitahidi kuyaweka kwenye menu ya African Festival mwaka huu

    ReplyDelete
  9. Masangu hayoo!! Mimi hushushia na CHAI YENYE SUKARI(hapa namchokoza Yasinta). Usukumani twayapika kwa Karanga..

    Mzee wa Changamoto umenifurahisha kweli.(Mama P, hapiki, anayetengeneza..

    ReplyDelete
  10. Aaah jamani umenikumbusha mbali sana..Hayo yananoga kwa chai bwana weeee.

    ReplyDelete
  11. Da Mija - MASANGU hayo yakitiwa karanga na maziwa kidogo kwa mbali we acha tu. Mtu unakuwa na nguvu za kulima shambani hata kwa masaa manane bila kusikia njaa!!!

    ReplyDelete
  12. Heri mimi sijasema...mmh! Mmmmh, yapo hayo na yale unayoweza kuchangaya na amziwa mgando...Mt yanaitwaje yale..KIBULU!

    ReplyDelete
  13. Prof. Matondo, nimekupata yaani wee acha tu. Hivi Rachel unajua/weza kulima?

    ReplyDelete
  14. hahahha jamani Mija kwani unanionaje kwikwikwi nawethaaaaaaa!
    Mija basi nami nataka kuonja hayo MASANGU YENU MANAYO KUMBUSHANA NA KAKA sasa niandike jina gani ok kaka Matondo lakini maziwa mmhhhh ok nitajaribu!

    jamani nawethaaa kulimaaaa miye yakhee!

    ReplyDelete
  15. Wapendwa nimegundua chakula cha Nyumbani kizuri na watu wanapenda sana vyakula vilivyo tulea!!!!

    @kaka Kitururu makande ya sukari mazuri jaribu bwana mimi ni mmoja wa wanaokula na sukari!!


    @NN Mhango hahhaa pole kaka yangu kwakukushusha mimate nakupa changa moto usiyasahau bwana mwambie Wifi apike ili umkumbuke mama!!

    @kaka Mubelwa hahaha mama p hapiki eheee anayatengeneza,mpe 5 Wifi wa mimi mama p!!
    @ kaka Matondo na da Mija natakanijaribu na maziwa hayo Masangu!!!!!!!

    @da Edna usilie wangu pika bwana wewe mwanamke wa kukaye!!
    @da Mumyheru utakuwa umewatendea wema kweli kwenye Africa Festival!!!
    @emu-three umeguna mwisho umesema, kibulu si mchezo!
    @Anonymous mimi huwa napika sana kwangu haikuwa sherehe wewe karibu sana tuu!!

    jamani nimefurahi mno kwa tafsiri ya Makande ukijua hivi na wengine wanajua hivi!
    MAONI HAYAJAFUNGWA NILIKUWA NAUNGA MKONO WOTE NA NAWAPENDA!!TUENDELEE KULA MAKANDE/MAKINDI/KIBULU/MASANGU/KITHERI N.K!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Napenda sana pure na sukari yummy

    ReplyDelete
  17. @M3: Kibulu mara nyingi hutengenezwa kwa maindi mabichi! Namaanisha mahindi ambayo hayajakauka bado!

    ReplyDelete
  18. @Rachel:Makande ya sukari nimejaribu hasa kwa kuwa DADA yangu nayemfuata kuzaliwa ndio apendavyo. Ila mie ya chumvi ndio nimeyazoea na naamini BIBI yangu mzaa Baba ni miongoni mwa wataalamu wakuyapika/kuyatengeneza aliye kiboko kuliko wapishi wote wa hiyo kitu.:-)

    ReplyDelete
  19. Jamani makande haya mie yanitoa roho! Wewe mtani wangu naona wataka kesi kutuwekea hii picha. Mie nakusubiria Fotobaraza. LOL...

    Mama Malaika

    ReplyDelete
  20. umeona da Lisa ehh utamu wake weee!
    @kaka Kitururu dada anajua utamu wake huyo!
    @mama Malaika!!!!!!!mataniusinipeleke mahakamani jamani mtani!nimefurahi kukuona ok tutakutana foto baraza!
    wewe na da Yasinta ni ndugu?maana upendo wenu na tabia zenu zinafanana sana!!.

    ReplyDelete
  21. Rachel Watu mnaweza kuwa na upendo pia tabia sawa lakini si ndugu huwa inatokea tu...Au labda ni ndugu ngoja tusubiri Mama Malaika atasema nini. Ila wewe mchokozi kweli na hayo makande na Mija ndo kabisa eti atamezea haya makande na chai ya sukari:-(...lol

    ReplyDelete
  22. jamani pure hizo mwe zina nikumbusha mbali mimi nimetoroka shule niende nyumbani nikale chakula kizuri weekend unafika nyumbani wana hamu ya pure wamejipikia pure zao unapiga hodi kina pakuliwa duuuuuuuuuuuuuuuuu pure umekimbia harage shule nyumbani pure linapendeza machoni ila du ndio umetoka shule na nyumbani pure tena mbona chozi lilinidondoka umenikumbusha mbali sana da Rachel ila jamani pure ndio zenyewe.

    ReplyDelete
  23. @Anonymous utoro wote ulikuisha maana adhabu ya kula hichohicho ilikutosha sana!!hahaha pure juu mpendwa!

    karibu sana wangu!.

    ReplyDelete