![]() |
| Wapendwa Nimatumaini yangu Jumapili hii ilikuwa/Inaendelea Vyema Nawataki kila lililojema,Amani,Furaha,Baraka na Fanaka. Utukufu tumarudishie MUNGU. |
5 Mwenyezi-Mungu ni mwema;
fadhili zake zadumu milele,
na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Neno La Leo;Zaburi 100
Wimbo wa sifa
(Zaburi ya shukrani)
1Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote!
2Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha,
nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!
3Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu.
Yeye ndiye aliyetuumba, nasi ni mali yake;
sisi ni watu wake, ni kondoo wa malisho yake.
4Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani,
ingieni katika nyua zake kwa sifa.
Mshukuruni na kulisifu jina lake.
5 Mwenyezi-Mungu ni mwema;
fadhili zake zadumu milele,
na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Bible Society of Tanzania
Bible Society of Tanzania
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Ni matumaini yangu nawe na familia pia wote waliokuzunguka mmekuwa na jumapili njema sana. Binafsi iliishia mzigoni:-)
ReplyDeleteAsante Kakdala wa mimi, ilikuwa njema.
ReplyDelete