Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 20 January 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo 2..


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamajambo Wapendwa/Waungwana?
Natumaini wote mmeamka salama na Mungu yu pamoja nanyi kwa kila jambo,
Yeye ni mwanzo kwetu na yeye ni mwisho kwetu hakuna wa kufanana naye.
Aendelee kuwabariki kuingia kwenu na kutoka kwenu,Akamguse kila mmoja
anayepitia magumu..Mungu akaonekane kwenye mapito,Shida/Tabu.
Akabariki kazi zetu na kuwaongoza wanafunzi katika masomo yao wakumbuke yote wanayofundishwa na kuelewa.
Mungu atosha..!!!!
Muwe na Wakati mwema.

     Mwanzo 2:1-25
1Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo. 2Siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Mungu akapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya. 3Mungu akaibariki siku ya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alipumzika baada ya kazi yake yote ya kuumba. 4Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa.
Bustani ya Edeni
Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 5Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. 6Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. 7Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.
8Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni, upande wa mashariki, na humo akamweka huyo mwanamume aliyemuumba. 9Mwenyezi-Mungu akaotesha kutoka ardhini kila aina ya miti mizuri izaayo matunda yafaayo kwa chakula. Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti wa uhai na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
10Kulikuwa na mto huko Edeni uliotiririka maji na kuinywesha hiyo bustani; kutoka huko mto huo uligawanyika kuwa mito minne. 11Jina la mto wa kwanza ni Pishoni; huo waizunguka nchi yote ya Hawila ambako kuna dhahabu. 12Dhahabu ya nchi hiyo ni safi kabisa. Huko pia kuna marashi yaitwayo bedola na vito viitwavyo shohamu. 13Jina la mto wa pili ni Gihoni; huo waizunguka nchi yote ya Kushi. 14Jina la mto wa tatu ni Tigri, nao watiririkia upande wa mashariki wa nchi ya Ashuru; na jina la mto wa nne ni Eufrate.
15Basi, Mwenyezi-Mungu akamtwaa huyo mwanamume, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. 16Mwenyezi-Mungu alimwamuru huyo mwanamume, “Waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani; 17lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.”
18Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Si vizuri huyu mwanamume kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” 19Basi, kutoka katika udongo, Mwenyezi-Mungu akaumba kila mnyama wa porini na kila ndege wa angani, halafu akamletea huyo mwanamume aone atawapa majina gani; na majina aliyowapa viumbe hao, yakawa ndio majina yao. 20Basi, huyo mwanamume akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, wanyama wa porini na ndege wote wa angani. Lakini hakupatikana msaidizi yeyote wa kumfaa.
21Basi, Mwenyezi-Mungu akamletea huyo mwanamume usingizi mzito, na alipokuwa usingizini, akatwaa ubavu wake mmoja na kupafunika mahali pale kwa nyama. 22Na huo ubavu Mwenyezi-Mungu alioutoa kwa yule mwanamume akaufanya kuwa mwanamke, akamleta kwa huyo mwanamume. 23Ndipo huyo mwanamume akasema,
“Naam! Huyu ni mfupa kutoka mifupa yangu,
na nyama kutoka nyama yangu.
Huyu ataitwa ‘Mwanamke’,
kwa sababu ametolewa katika mwanamume.”
24Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake, akaambatana na mkewe, nao wawili huwa mwili mmoja.
25Huyo mwanamume na mkewe wote walikuwa uchi, lakini hawakuona haya.
Mwanzo 2:1-25
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (BHN): 
Jifunze zaidi

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 19 January 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Tuanze na Mwanzo

Shalom,Hamjambo Wapendwa/Waungwana?
Nimatumaini yangu mmeamka salama..
Sifa na Utukufu ni kwake Mungu Baba.
Wagonjwa,wenyeshida/Tabu Mungu akawaguse,
Tukaanze siku  na Mungu ,Atubariki,Atulinde,Atuongoze katika yote.
Muwe na wakati mwema.

               
Kuumbwa Ulimwengu


“Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji. Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza. Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.” Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo. Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili. Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo. Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema. Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu. Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka, na ingae angani na kuiangazia dunia.” Ikawa hivyo. Basi, Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; ule mkubwa utawale mchana na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka mianga hiyo angani iiangazie dunia, ipate kutawala mchana na usiku, na kuutenga mwanga na giza. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya nne. Mungu akasema, “Maji na yatoe makundi ya viumbe hai na ndege waruke angani.” Basi, Mungu akaumba wanyama wakubwa sana wa baharini na aina zote za viumbe vyote hai viendavyo na kujaa majini; akaumba na aina zote za ndege wote. Mungu akaona kuwa ni vyema. Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni, muongezeke, muyajaze maji ya bahari; nao ndege waongezeke katika nchi.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tano. Mungu akasema, “Nchi na itoe aina zote za viumbe hai, wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo na wanyama wa porini wa kila aina.” Ikawa hivyo. Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema. Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.” Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya sita.”
Mwanzo 1:1-31 BHND
http://bible.com/393/gen.1.1-31.bhnd

"Swahili Na Waswahili"Mabarikiwe.

Wednesday 18 January 2017

Anza Nami Baba;Kikombe Cha Asubuhi....

Shalom,Habari za Asubuhi,Habari zenu,Hamjambo,Mmeamkaje,.......
wewe umezoe kutoa salam ya vipi?

Tunamshukuru Mungu kwakutuamsha salama na wenye Afya,Asante Mungu
kwa kutupa kibali cha kuiona tena siku hii, Sisi si kwamba ni wema sana,
Tunapokea kutoka kwako kwa Neema tuu..
Basi Baba ukatuongoze Kwenye Kunena na kutenda, Tuingiapo na tutokapo,Kwenye Vyombo vya Usafiri,
kwenye kula na kunywa,Baba Tunaomba Ukabariki kazi zetu na ukawaongoze watoto/wanafunzi kwenye masomo yao.
Ukawaguse wenye Shida/Tabu,Wagonjwa walio mahospitalini na Majumbani,Yatima na Wajane,
Walio magerezani pasipo na hatia,Mfalme wa Amani ukatawale kwa kila jambo.
Ameeeen.
Anza na Mungu Baba..!!!!




““Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani. Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo; “Miji yenu itabarikiwa na mashamba yenu. “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi. “Vikapu vyenu vya nafaka vitabarikiwa na vyombo vyenu vya kukandia. Mtabarikiwa mnaporudi nyumbani na mnapotoka nje. Maadui zenu wakiwashambulia, Bwana atawapeni ushindi juu yao. Wakija kuwashambulia kwa njia moja watawakimbieni kwa njia saba. Baraka za Mwenyezi-Mungu zitakuwa katika ghala zenu za nafaka na katika shughuli zenu zote. Atawabariki katika nchi ambayo anawapeni. “Mwenyezi-Mungu atawafanyeni kuwa watu wake watakatifu kama alivyowaahidi, kama mkizitii amri zake yeye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kufuata njia zake. Mataifa yote duniani yakiona kwamba nyinyi mnaitwa kwa jina la Mwenyezi-Mungu yatawaogopa. Mwenyezi-Mungu atawafanikisha kwa wingi: Watoto, mifugo na mavuno shambani katika nchi aliyowaapia wazee wenu kuwa atawapeni, Mwenyezi-Mungu atawafungulieni hazina yake nzuri kutoka mbinguni na kunyesha mvua katika nchi kwa wakati wake, na kubariki kazi zenu. Mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza, bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.”
Kumbukumbu la Sheria 28:1-14 BHND
http://bible.com/393/deu.28.1-14.bhnd

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 17 January 2017

Saalam za Mwaka Mpya Wapendwa/Waungwana...Muwe na wiki Njema yenye Baraka..(Hata mimi nasema yu mwema Mungu)Burudani Atosha Kisaava..!!!


Habari za siku Wapendwa/Waungwana,Heri ya Mwaka Mpya.!!!
natumaini wote mmeupokea vyema na Mungu aendelee kututendea sawa sawa na mapenzi yake.
Yeye yu Mwema sana, Ije mvua lije Jua atabaki kuwa Mungu..
Ukikosa,Ukipata endelea kumuomba Na Kumtukuza yeye tuu maana yeye Atosha.
Tupo pamoja Wapendwa /Waungwana..ni mambo yanaingiliana tuu,kikubwa uzima...

AHADI YA MUNGU NI YA KWELI



              Neno La Leo;Waebrani 6:13-20

Ahadi ya Mungu ni ya kweli
13Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa. 14Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” 15Abrahamu alisubiri kwa uvumilivu na hivyo akapokea kile alichoahidiwa na Mungu. 16Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu kuliko wao, na kiapo husuluhisha ubishi wote. 17Naye Mungu aliimarisha ahadi yake kwa kiapo; na kwa namna hiyo akawaonesha wazi wale aliowaahidia kwamba hatabadili nia yake. 18Basi, kuna vitu hivi viwili: Ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.19Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni. 20 Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.



"Swahili Na Waswahili"Mungu yumwema, Mbarikiwe.

Sunday 11 December 2016

Niwatakie Jumapili hii iwe Njema kwenu;Kwaya ya Mamajusi (Mamajusi Choir) - Tunalindwa na Nyingine..


Wapendwa/Waungwana;Ni matumaini yangu Mungu anawalinda na amewaamsha salama,
Wenye shida/Tabu Mungu akawaguse na kuwaponya katika yote...
Yeye ni kila kitu,Tumaini,Upendo,Uponyaji,Utukufu,Baraka,Amani,Furaha vipo kwakwe Muumba
Mbingu na nchi...yeye Atoshaa!!!!















Neno La Leo;Wakolosai:3;5-17 Na Yakobo:3;1-18



Wakolosai:3:5-17

Maisha ya kale na maisha mapya
5Basi, ueni chochote kilicho ndani yenu ambacho ni cha kidunia: Uasherati, uchafu, shauku, tamaa mbaya na uchu (ambao ni sawa na kuabudu sanamu). 6Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya Mungu huwajia wote wanaomwasi. 7Wakati mmoja nyinyi pia mliishi kufuatana na mambo hayo, mlipotawaliwa nayo. 8Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: Hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu. 9Msiambiane uongo, kwani nyinyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, 10mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu. 11Katika hali hii, hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, msomi na asiye msomi, mtumwa na mtu aliye huru. Kristo ni kila kitu, na yumo katika yote.
12Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi. 14Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili. 15Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani! 16Ujumbe wa Kristo na ukae ndani yenu pamoja na utajiri wake wote. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Mungu mioyoni mwenu kwa shukrani. 17Na, kila mfanyacho kwa neno au tendo, fanyeni vyote kwa jina la Bwana Yesu na kumshukuru Mungu Baba kwa njia yake.






Yakobo:3;1-18

Ulimi
1Ndugu zangu, wengi wenu msiwe waalimu. Kama mjuavyo, sisi waalimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine. 2Lakini kama mtu hakosi katika usemi wake, basi, huyo ni mkamilifu, na anaweza kutawala nafsi yake yote. 3Sisi huwatia farasi lijamu kinywani mwao ili watutii; na kwa njia hiyo twaweza kuwaongoza kokote tunakotaka. 4Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka. 5Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana.
Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa. 6Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe. 7Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe vyote – wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini. 8Lakini hakuna mtu aliyefaulu kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua. 9Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huhuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu. 10Maneno ya kubariki na ya kulaani hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo. 11Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja? 12Ndugu zangu, je, mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.
Hekima itokayo juu mbinguni
13Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima. 14Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli. 15Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani. 16Maana popote palipo na wivu na ubinafsi, hapo pana fujo na kila aina ya uovu. 17Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki. 18Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani.
Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe sana.

Saturday 10 December 2016

Jikoni Leo; Na da'Fathiya (Aroma of Zanzibar)UNGA WA PUFF PASTRY - KISWAHILI





Mahitaji 1

Siagi vikombe 3
Unga wa ngano kikombe 1

Mahitaji 2

Unga wa ngano vikombe 4
Chumvi vijiko 2 vidogo
Maji ya ndimu kijiko 1 kidogo
Maji ya baridi kikombe 1
Siagi 1/2 kikombe


Shukrani;
Aroma of Zanzibar

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Tuesday 6 December 2016

TANZIA: MAREHEMU FELIX KAPINGA ATAZIKWA LEO TAREHE 06/12/2016 MKOANI NJOMBE


Marehemu Felix Kapinga enzi za uhai wake. 

Wanajumuia ya wanafunzi waliosoma Tumaini University - Iringa, Songea Boys High School na Lugalo Secondary School wanasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa mwanafunzi mwenzao Marehemu Felix Kapinga kilichotokea Usiku wa Tarehe 3/12/2016 katika Hospitali ya Ikonda Mission Mkoa wa Njombe baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
Tunachukua fursa hii kutoa pole kwa Mke wa marehemu, Mtoto wa marehemu, Mama mzazi wa marehemu, wafanyakazi wenzake kutoka Njombe community Bank, Ndugu, jamaa, Marafiki na wana familia kiujumla kwa msiba huu walioupata, tunaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo tarehe 06/12/2016 huko huko Njombe katika eneo la kijiji kinachotambulika kwa jina la Ramadhani  ambako Mama mzazi wa marehemu ndiko anakoishi, shighuli za Mazishi zinategemewa kufanyika kuanzia saa 6.00 Mchana. Kwa taarifa zaidi unaweza ukawasiliana kwa namba 
+255 713 254553

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMIN.