Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 10 November 2016

Mswahili Ni Nani?
















Shukrani;mtembeziTV


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

New comment ya Ras choyo on Wanaume na Mitindo,Leo wenye Rasta Eti!!!!!!!.(hizo sio Rasta, hivyo ni vishungi/vifundo ama......)soma zaidi







kuona post ingia hapa; 
http://swahilinawaswahili.blogspot.com/2011/06/wanaume-na-mitindoleo-wenye-rasta-eti.html?showComment=1478354804495#c4462530939513813249 "Wanaume na Mitindo,Leo wenye Rasta Eti!!!!!!!":

hizo sio Rasta, hivyo ni vishungi/vifundo ama dread kwa kizungu. Rasta ni kifupisho cha Rastafarian ambayo ni imani inayoamini kwamba mfalme Haile Selasie ndiye Masihi/masiya (Ras Tafar ni jina halisi la Haile selasie kabla ya kuwa mfalme, alipewa jina la haile selasie lenye maana ya 'nguvu ya utatu mtakatifu' mara baada ya kushika ufalme wa ethiopia, hii ni sawa na mapapa wa kanisa katoliki hupewa majina mengine kama vile John, benedict, baada ya kupewa u-papa). Rastafarians huamini kwamba bustani ya Eden iko ethiopia kwani ufafanuzi wake kwenye kitabu cha MWANZO unatoa ushahidi kuwa ni ethiopia kwani jina KUSH limetajwa (soma Mwanzo kwa uhakika zaidi) vile vishungi vya nywele hufugwa muumini wa Rastafari anapoingia kwenye nadhiri ya kumtumikia Mungu kwenye maisha yake yote (rejea jinsi samson wa kwenye biblia alivyowekewa nadhiri ya kumtumikia Mungu na kuamriwa kutonyoa nywele)



Posted by Ras choyo to Swahili na Waswahili at 5 November 2016 at 14:06


Asante kwa mawazo/mchango wako kaka Ras Choyo
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 7 October 2016

Mahojiano na Mhe Peter Serukamba nchini Marekani


Karibu na asante kwa kujiunga nasi
Oktoba 6, 2016, tulipata fursa ya
kutembelewa studioni (Kilimanjaro Studio, Beltsville, Maryland) na
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Tumejadili mengi tu kuhusu Tanzania yetu
KARIBU

Mahojiano na Rahima Shaaban. Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Ubunifu wa Beautiful Jamila




Kwanza Production

 Beautiful Jamila ilianzishwa mwaka 2013 na Rahima Shabani na makao makuu ni Atlanta Georgia.

Inajihusisha na harakati za kutangaza tamaduni za kiSwahili na kiAfrika.

Mwanzilishi wake aliungana nasi studio kuzungumza mengi kuhusu yeye, kampuni yake na tamasha lijalo




Wednesday 21 September 2016

Kipindi cha Reggae Time Pride Fm Sept 17 2016.....Mahojiano na Innocent Galinoma


Karibu katika kipindi cha REGGAE TIME ya Pride Fm Mtwara Tanzania.

Na leo, ni mazungumzo yangu na Innocent Galinoma ambaye alikuwa mkarimu sana kufika Kilimanjaro Studios kwa mahojiano.



Ni kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, mbili kamili kwa Marekani Mashariki

Jiunge nasi kupitia 87.8 Fm kwa mikoa ya kusini, ama www.878pridefm.com ama kupitia TuneIn, bofya tun.in/seTTx.

Tuesday 13 September 2016

Kipindi Cha Jukwaa Langu Sep 12 2016....Tetemeko Bukoba


Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo, tulizungumzia janga kuu la Tetemeko la ardhi nchini Tanzania
Wadau
Baraka Galiatano wa BukobaWadau Blog na Erick Kimasha walijiunga nasi
kwa njia ya Skype kutoka Tanzania kutupa taswira ya nini kilitokea, vipi
kilipokelewa na maendeleo tangu Sept 10 na hali ilivyo hivi sasa mjini
humo.
Pia tuliungana na mmoja wa wanaharakati ambao wameanzisha mfuko maalum kuchangia wahanga wa tetemeko hilo Agnetta .



Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093

Karibuni

Tuesday 30 August 2016

Kipindi cha JUKWAA LANGU Aug 29 2016 (Pt 1)...Demokrasia Tanzania


Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA ya sasa na ile tuitakayo.

Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania na ukuaji wa Demokrasia ya nchi yetu.

KARIBU