Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 18 April 2016

MWILI WA MAREHEMU HENRY KIHERILE WAAGWA HOUSTON, TEXAS


Jioni ya jana Jumamosi (16/04) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada Takatifu katika kanisa la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. Mwili wa marehemu Henry unatarajiwa kusafirishwa jioni ya leo kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.

Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake
Gari lililobeba mwili wa Henry likiingia kanisani


Wachungaji wakiwa nje ya kanisa kabla ya ibada


Jeneza lililobeba mwili wa Henry likiingizwa kanisani
Dada  Lulu  ( mdogo wa Marehemu Henry ) akimuaga kwa uchungu kaka yake
Mr. & Mrs. Tenende ( Baba na Mama mkubwa wa marehemu ) wakiwa kanisani
Waombolezaji wakilia kwa uchungu
Rafiki wa Henry kutoka Cameroon
Waombolezaji



























































































Friday 15 April 2016

Kisa cha Leo na Tweve Hezron



Bosi wangu alikuwa akitembelea gari nzuri sana na kila siku ilikuwa ni kazi yangu kumfungulia mlango na kumsalimia.

Lakini tokea niajiliwe na mke wake kuwa kama mlinzi pale kwao hakuwahi kupokea salamu yangu hata siku moja. Nilimuona ananidharau sana ila sikuwa na jinsi.

Siku moja wakati akitoka ndani aliniona nje nikitafuta kama kuna chakula kilichobaki katika dustbean. Lakini kama kawaida yake alinitizama mara moja akaendelea na shughuli zake.

Siku iliyofuata niliona mfuko wa rambo palepale kwenye zile dustbean (ndoo za takataka), ila mifuko ile ilikuwa misafi mno na ndani kulikuwa kuna chakula kizuri tu ambacho pasina shaka nilijua tu kitakuwa kimetoka supermarket.

Sikujiuliza ni nani ametupa me nilifurahi kukipata. Kila siku nikawa nikiona mfuko wa rambo hapo kwenye dustbean ukiwa na vyakula vizuri. Hii ikawa ni utaratibu wa kila siku. Nami sikuuliza ni nani amekuwa akiweka.

Jioni ninaporudi nyumban kwenye makazi duni niliyokuwa nikiishi na familia yangu, nilirudi nacho na nikawa nakula na kushare hicho chakula na familia yangu.

Nikashangaa sana ni nani mpumbavu ambae anatupa chakula kizuri kama kile kila siku? Ila nikajijibu mwenyewe kwamba kuna gepu kubwa sana kati ya masikini na tajiri, wala sikujihangaisha kuuliza.

Siku moja kulikuwa na tatizo kubwa mahala nilipokuwa nikifanya kazi. Niliambiwa kuwa bosi wangu amefariki. Kulikuwa na wageni wengi sana waliokuja pale nyumbani na siku hiyo sikupata chakula katika zile dustbean kama kawaida.

Hivyo nikajua labda mmoja wa wageni labda alikiona na akachukua. Ila hali hiyo ikaendelea kujitokeza baada ya shughuli za msiba kuisha na hata week zingine zilizoendelea sikupata kitu. Na nikaona hali imekuwa ngumu tena kuihudumia familia yangu chakula kwa kuwa nilishakuwa nimewazoesha kuwaletea kila jioni.

Hivyo nikaamua kumuomba mke wa marehemu bosi wangu kwamba aniongezee mshahara ama vinginevyo niache tu kazi maana hali ilikuwa ngumu.

Baada ya kumueleza hilo alilalamika kwanini sikulalamika suala la mshahara miaka miwili sasa imeshapita nije nilalamike leo, kwanini mshahara usitoshe leo? Nilimpa sababu nyingi ila hazikumshawishi hata kidogo.

Mwishoni nikaamua kumueleza ukweli, nikamueleza ishu nzima ya mimi kupata chakula cha bure pale kwenye dustbean na kwa jinsi gani kilinisupport kuilisha familia yangu. Pia nikamueleza kukikosa kwa muda sasa.

Akaniuliza ni lini ilikuwa mwisho wa kukipata hicho chakula katika dustbean? Nikamueleza kuwa baada ya kifo tu cha mumewe sikupata tena chakula.

Nikajiuliza kimyakimya mbele yake, Je inamaana bosi wangu ndio alikuwa akinikiwekea kile chakula kila siku? Hapana sidhani maana kwa jinsi alivyokua akinidharau kwa kutopokea salamu zangu asingekuwa na ubinadamu wa kunipa chakula.

Mke wa bosi wangu akaanza kulia, nikamuomba anyamaze na nikamuomba radhi kwa kumuomba aniongezee mshahara.

Mke wa bosi akaniambia, ninalia kwa sababu nimempata mtu wa saba ambae mume wangu alikuwa akimsaidia kumpa chakula fresh toka supermarket kila siku.

Nilikuwa najua mume wangu anawasaidia chakula watu saba wasiojiweza kila siku, ila nilipata kuwafahamu sita tu. Na siku zote nilikuwa nikitaka nimjue wa saba alikuwa nani ili niendelee kutoa huduma ambayo mume wangu amekuwa akiifanya. Nimefurahi kwa kuwa kumbe ndio wewe!

Kuanzia siku ile nikaanza kupokea chakula tena kama kawaida, ila safari hii mwanae wa kiume ndio alikuwa akituletea nyumbani.

Ila kila nilipokuwa nikimshukuru hakuwahi kunijibu! Kama baba yake tu!

Siku moja alinipa chakula pale nyumbani kwao nikamwambia AHSANTEE kwa sauti ya juu sana, akabaki ananishangaa. Mama yake akatoka nje akaniambia usijisikie vibaya akiwa hakujibu ni kiziwi kama baba yake alivyokuwa kiziwi. Akanieleza kuwa mumewe alikuwa ni bubu pia kiziwi na huyo mwanae nae yuko hivyohivyo.

Nilisikitika sana kwa jinsi nilivyokuwa nikiwawazia vibaya, tofauti na jinsi walivyo.

_______________________________________

Oh! Tumekuwa tukikosea mara nyingi sana kuwahukumu wenzetu bila kujua ni nini nyuma ya kile wanachokifanya. Kuwa na busara katika kuishi na wanadamu wenzako, huwezi jua kila mmoja wetu anapigana vita ngumu.

Kuwa makini, sio kila kitu unajitizama wewe peke yako kabla huja assume mambo ni bora ukauliza. Usikimbilie kutoa maamuzi kabla hujachunguza jambo, huenda siku ukaumia au kupatwa jambo lolote lile baya.

Matatizo mengi katika jamii zetu yanasababishwa na jinsi sisi wenyewe tunavyowachukulia wenzetu. Usihukumu hali fulani ambayo hujawahi kuipitia. Kuwa na busara ya kujifunza, huwezi kujua vyote.

Kuanzia leo tubadili fikra mbaya juu yetu na kwa wenzetu. Kuna vitu viwili katika hadithi hii mosi, usiamini kila unachoambiwa, chunguza zaidi. Na cha pili tambua kwamba kila mmoja unaekutana nae anapigana vita ambayo wewe huijui.

Hima, tuifanye Dunia kuwa mahala salama pa kuishi.

Share

Tweve Hezron

Thursday 14 April 2016

MBUNGE WA CHAMA CHA WAZALENDO ACT-TANZANIA AKUTANA NA WATANZANIA NEW YORK CITY



Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New York. Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo wake juu ya kasi ya rais wa wamu ya 5. Zitto ni mmoja ya vijana kwenye Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na uwezo wa kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na kuitikisa serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye ndiyo alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala. Na pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University  New York na kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard University huko Boston. MA.  Picha na Vijimambo Blog New York
Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira   zaidi nenda soma zaidi.

Zitto  akitafakari swali kabla kujibu,  Zitto aliulizwa kama yupo tayari kuungana na Ukawa na kama yupo tayari kungombea kiti cha urais kupitia chama chake ACT, majibu yalikuwa yupo tayari kuungana na ukawa lakini anaitaji kujua nini faida ya kuungana na kama kuungana ili kuing'oa CCM basi iwe na nguvu kweli kweli na ifanikiwe kwani asinge penda kuungana na nakubakia msindikizaji tu bila faida endelevu na kama yupo tayari kugombea kiti cha urais basi atafanya hivyo akiwa amesha jiandaa vilivyo ili akigombea apata ushindi wa kishimdo na kuing'oa CCM na siyo vinginevyo.

Hapa ni Patel akiuliza swali kwa Zitto,  Patel ni Mtanzania mwenye asili ya India ndiyo aliandaa mkutano huu kwa kushirikiana na Nasaan Chiume.

Shabani Mseba akiuliza swali kwa Zitto swali lake nini mipango ya maendeleo jimboni kwake.
Na jibu lake lilikuwa  mipango yake ni kuhakikisha  elimu  inakuwa na mwamko ndani ya mkoa wake. Kwani elimu imeshuka sana na ufaulu wa watoto umezidi kuwa chini.

Wednesday 6 April 2016

[VIDEO] Mahojiano ya Mubelwa Bandio na mgombea uwakilishi nchini Marekani Will Jawando

Photo Credits: @wjawando
Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando
alihojiwa na Mubelwa Bandio katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland
nchini Marekani. Mbali na mambo mengine, alizungumzia kuhusu mikakati yake katika
kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla. Ikumbukwe kwamba 10% ya wazaliwa wa Afrika wanaoishi Marekani, wapo katika jiji la Washington DC

Karibu ufuatilie mahojiano haya