Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 4 November 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 2, 2015 (Full Show)


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.
Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya UCHAGUZI MKUU 2015


Monday 2 November 2015

[PICHA]: MISA YA MAREHEMU MAMA GREN JUDICA MOSHI Washington DC


Ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC

Watoto wawili wa Marehemu Donald na James Moshi, na ndugu wengine, waliungana kwa misa hiyo iliyofanyika alasiri na kufatiwa na chakula cha pamoja

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries Ferdnand Shideko, akiwakaribisha watu waliohudhuria misa hiyo

Mch John Kadyolo akifungua misa kwa maombi

 Wanafamilia

[PICHA] Utambulisho wa kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili Washington DC


Jumamosi,Oktoba 31, Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV hapa Marekani.
Pia, Swahili Media Network inaandaa kipindi cha Radio cha Jambo America, kinachosikia kupitia WJFK ambayo ni radio-dada ya WPGC chini ya shirika la CBS Radios

Ratiba kamili ya vipindi kutoka Swahili Media Network, itawajia hivi karibuni

Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo

Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme (wa pili kushoto) ambaye pia alimuwakilisha Mhe Balozi Wilson Masilingi, akimsikiliza mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza

Steven Mghaza akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi, na mwakilishi wa balozi kwenye hafla hiyo, Swahiba Mndeme
Kushoto ni Meneja mauzo wa CBC Radio R.J Trzaska, mratibu wa Mis Congo na msanii toka congo

Mshereheshaji wa siku hiyo, Grace Ssebo akikaribisha wageni

Wasanii Adele na Frank wakiimba nyimbo za taifa za Marekani na Tanzania, wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo

Mwakilishi wa balozi, ambaye pia ni Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme, akisalimia wageni wakati wa utambulisho

Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme akitambulisha rasmi kipindi hicho

Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska

Mmoja wa washiriki wa Jambo Show Radio inayotayarishwa na Swahili Media Network, Sala Damali

Mwanzilishi wa Jambo Show Steven Mghaza akielezea kipindi hicho kwa wageni waalikwa
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska akielezea umuhimu wa radio kwa jamii yetu na muelekeo wake

Sunday 1 November 2015

IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU GODFREY MNGODO, COLUMBUS, OHIO


Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu
Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini
Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa
kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu
Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na
kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu
mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America,
wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA
KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO
Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin
wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu
Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini
Marekani.
Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.
Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake
Alvin.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa Picha zaidi bofya HAPA

Tuesday 27 October 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Okt 26 2015 (FULL)


Photo Credits: dw.com/sw


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Na leo, tulizungumzia Tanzania baada ya Uchaguzi wa jana Oktoba 25, 2015

Sunday 25 October 2015

Nawatakia Jumapili Njema na Uchaguzi mwema ;Tanzania Kwanza,Burudani-Kinondoni Revival Choir Twalilia Tanzania

Wapendwa/Waungwana natumai hamajambo na Jumapili hii ya Uchaguzi Tanzania ni njema..
Mungu azadi kuibariki Tanzania na Watanzania katika yote,Uchaguzi uwe wa haki,Amani,Utulivu.
Amani,Upendo,Umoja,Mshikamano,Undugu,Hekima,Busara vikatawale...
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.


1Ndugu zangu, ninataka na kutazamia kwa moyo wangu wote hao wananchi wenzangu wakombolewe. Tena nawaombea kwa Mungu daima. 2Maana naweza kuthibitisha kwa niaba yao kwamba wanayo bidii ya kumtafuta Mungu; lakini bidii hiyo haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli. 3Maana hawakufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu wawe waadilifu, na wamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe na hivyo hawakuikubali njia hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu. 4Maana kwa kuja kwake Kristo, sheria imefikia kikomo chake, ili wote wanaoamini wafanywe waadilifu.

Neno La Leo;Warumi 10:1-21
Ukombozi kwa wote
5Kuhusu kuwa mwadilifu kwa kuitii sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya sheria ataishi.”6Lakini kuhusu kuwa mwadilifu kwa njia ya imani, yasemwa hivi: “Usiseme moyoni mwako: ‘Nani atapanda mpaka mbinguni?’ (yaani, kumleta Kristo chini); 7wala usiseme: ‘Nani atashuka mpaka kuzimu?’ (yaani, kumleta Kristo kutoka kwa wafu).” 8Maandiko Matakatifu yasema hivi: “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri.9Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. 10Maana mtu huamini kwa moyo akafanywa mwadilifu; na hukiri kwa kinywa akaokolewa.11Maandiko Matakatifu yasema: “Kila anayemwamini hataaibishwa.” 12Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao. 13Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.”



14Basi, watamwombaje yeye ambaye hawamwamini? Tena, watamwaminije kama hawajapata kusikia habari zake? Na watasikiaje habari zake kama hakuna mhubiri?15Na watu watahubirije kama hawakutumwa? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari Njema!” 16Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17Hivyo basi, imani inatokana na kuusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
18 Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:
“Sauti yao imeenea duniani kote;
maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
19Tena nauliza: Je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu:
“Nitawafanyeni muwaonee wivu
watu ambao si taifa;
nitawafanyeni muwe na hasira
juu ya taifa la watu wapumbavu.”
20Tena Isaya anathubutu hata kusema:
“Wale ambao hawakunitafuta wamenipata;
nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.”
21Lakini kuhusu Israeli anasema:
“Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Tuesday 20 October 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Oct 19 2015 (Full)


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Ni kipindi cha mwisho kabla ya uchaguzi, na washiriki wengi walishiriki kutoa mchango wao kuhusu mchakato ulivyokuwa, na neno ama wosia wao kwa waTanzania wote

KARIBU