Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 31 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo,mambo ya Taarab-Utalijua Jiji!

Haya Waungwana mambo hayo, hahaaaa Mambo ya Taarab... Swahili na Waswahili twende Sote sasa!!

Thursday 29 March 2012

MAZISHI YA MAREHEMU DENIS OSWALD KAPINGA


Ndg. Joseph Oswald Kapinga

Ndugu Joseph Kapinga pichani hapo juu anapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kuwa Ratiba ya mazishi ya mpendwa mdogo wetu Denis O. Kapinga yatafanyika leo Tarehe 29/03/2012 katika makaburi ya Sinza karibu na ukumbi wa mwika.

Ratiba itakuwa kama ifuatavyo:

Mwili wa marehemu utafika Nyumbani maeneo ya Sinza karibu na New White Inn Bar bara bara ya Sinza uzuri mnamo saa 6.00 Mchana kutoka Hospitali ya Mwananyamala.

Mwili utaagwa nyumbani saa 7.00 Mchana na baadae utapelekwa kanisa la Roman Catholic Sinza kwa Ibada.

Baada ya hapo Saa 8.30 Mchana mwili wa marehemu utapelekwa Makaburi ya Sinza kwenye nyumba yake ya milele.

"BWANA ALITOA NA BWANA 

Poleni sana Familia ya Kapinga.
Swahili na Waswahili tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu kwenu.

Mungu awatie Nguvu.
Ulale kwa Amani kaka Denis.O.Kapinga.

Tuesday 27 March 2012

Jikoni Leo-Ni kwa Mama Mwakitalu!!!Pata na Burudani ya Ngoma!!!!![Mwanamke jiko au Mwaume Jiko?]



Da'Masika/mama Mwakitalu
Mboga za Majani Mchanganyiko,Majani ya Kunde na Majani ya Maboga
Mchuzi wa Samaki Umeungwa/wekwa Nazi na nyanyachungu

Maandaziiiiii na hapo chini ni Mahindi ya Kuchemsha.

Haya Waungwa,vipi wewe unapenda kupika?au Unapika kwasababu ni lazima upike na ule?Kwenye kazi za Nyumbani kila mmoja kuna kazi anapenda kuifanya, Na kuna baadhi ya Kazi hatuzipendi,Lakini tunafanya kwa sababu ni lazima zifanywe,Na utasikia duuh yule kaka/dada au Mama/Baba anajua Kupika sana,Hivi kujua kupika ni Chakula kiive au?
Kwani Utamu/Radha ya chakula wewe unaweza kupendezwa nacho na mwingine asipendezwe nacho.
Jee Kazi/Ujuzi wa Kupika ni kwa Wanawake tuu?Kwani mara nyingi utasikia Mwanamke jiko na si Mwanaume Jiko,Hasa kwa Maisha ya Leo,
 kwa Maisha ya Zamani wengi wao Mama/Dada kazi yao kubwa ni Upishi na Baba wengi ndiyo walikuwa wanafanya Kazi hasa Mijini, Kwa Vijijini Woote BABA na MAMA Wanaenda shambani lakini Kupika ni MAMA.Jee Leo Tunaweza Thubutu kusema MWANAUME JIKO? AU TUTAKUA TUMEWADHALILISHA?Kwani wapo Wanakarangiza haswaaaa kutushinda au Hamjakutana nao?.


Karibuni Waumgwana kwa Mawazo na Kuelimisha na Kwa upendo.

MWAKILISHI WA UNOPS NCHINI SIERA LEONE NDUGU OMARY MJENGA AKISALIMIANA NA RAIS KIKWETE WAKATI WA MAZISHI YA MKUU WA WILAYA YA LIWALE MAREHEMU VICTOR P. CHIWILE JANA KIBAHA.


Mmoja wa waombolezaji akimsalimia Rais Kikwete kwa kuibusi Pete yake, kulia ni Ndugu Omary Mjenga akishuhudia tukio hilo.
Rais akisalimiana na Ndugu Omary Mjenga jana walipokutana kwenye mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale.
Ndugu Mjenga alikuwa Personal Secretary wa Rais Kikwete wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje kabla hajawa Rais.

Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk/
Ahsante Sana.

Sunday 25 March 2012

Nawatakia J'Pili Njema Woote!!Burudani-AIC Chang'ombe Vijana Choir - Hakuna

Nawatakiaeni J'pili njema yenye kheri,Baraka,Upendo na Utu wema.
Neno la Leo;Zaburi ya 121:1-8.Nitayainua Macho yangu niitazame Milima,Msaada wangu Utatoka Wapi?Endelea.
Nijambo Gani linalomshinda MUNGU BABA?.

Saturday 24 March 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Twanga Pepeta - Mtu Pesa na nyingine nyingi!!!

Papaa Sunday, Yeye ndiyo aliyenianzishia wana Twangwa leo, Ahsante kaka yangu, Duhh Pia nimekumbuka Mengi sana Ndugu yangu. Papaa Huyu tumecheza nae sana Mpira wa Makaratasi,Makonzi , Hahahahhaaha Enzi za Masonge muuza Mihogo,Mzee wasiwasi ooohhiiii. Tumetoka mbali sanaaaaa!!Hili nitalikumbushia siku nyingine, Pata Burudani na Nawatakia J'mosi Njeeeeeemaaa!!!Mimi nawapenda Wooote Waungwana. Twende Sote sasa.Twanga pepeta Inapendaga Watu Woteeee ehhhh ohhhhh Ehhhheee!!!!!!!