Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Waswahili na maisha Yao. Show all posts
Showing posts with label Waswahili na maisha Yao. Show all posts

Thursday 15 September 2011

Waswahili Wetu Leo, Mkubwa na Wanawe/Miaka50 ya Uhuru!!!!!!!!

Haya Mpedwa wewe umejiandaaje na Miaka 50 ya Uhuru?
Sikiliza hayo maneno ya Waswahili, Chura anapenda Maji lakini si ya Moto.
Watoto wa Kiswahili wanatimbwilika/kucheza.Tanzania Kiroho Safi!!!!!!
Je wewe una Amani, Uko Huru? Kila la Kheri.

Wednesday 24 August 2011

Mswahili Wetu Leo ni Mh; Balozi Mama Mwanaidi wa Maajar!!!!!!!




Mh; Mama Mwanaidi  Maajar; Aliongea hayo kwenye Semina ya Kina mama wa THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES CHURCH.
Mpendwa baada ya kumsikiliza mama Maajar, Je  umejifunza nini?.Sikiliza kwa makini sehemu ya 1 na ya 2.

Karibuni sana kwa mawazo/maoni na kuelimishana zaidi katika kipengele hiki cha, Waswahili na Maisha yao ,Kupitia hapa Swahili naWaswahili.

Habari  kwa msaada wa DjLuke wa  Vijimambo.



Monday 15 August 2011

Waswahili wa Mji wa Cork,Ireland na Futari ya Pamoja!!!!!

                         Mji wa Cork katika picha.
     Wanawake wakipika na kina baba wakijiandaa kupokea wageni.
           Waandazi/waandaaji wakiwa tayari.
              Waswahili hawa nao walikuwepo.
         Watoto wa kiswahili wametulia.
   Shekhe akisisitiza Upendo na Umoja kwa Waswahili.
     Waswahili wakisaidiana ili mambo yawe sawa.
         Kina mama na kina kaka wakiendelea na maandalizi.
 Wakiendelea na Futari.
         
  Kina mama wakishughulika.
    Lete Uji hapa!
    Vipi mko sawa!
    Baada ya kumaliza msosi.
   Wakisikiliza maongezi.
    Watu wa karibu baada ya wageni kuondaka wakijipongeza!
                                      Maalim akitoa Shukrani kwa wote waliofika na wasiofika,Mungu awabariki sana na kuwaongezea kila lililo jema na Amani.Anawatakia Funga njema na anawapenda wote.

Shughuli hii ya Futari ya pamoja iliandaliwa na Maalim picha ya chini mwenye kanzu.Kwa kumshukuru Mungu na kuunagana na familia,pia kuwashukuru Wasawhili na jamaa zake kwa kuwa naye pamoja kwa kila jambo.

Thursday 4 August 2011

Mswahili Wetu Leo ni Bi Zaituni wa Mrisho; Anaishi ILALA!!!!!!!

Bi Zaituni wa Mrisho katika Picha ndiyo Mswahili wetu wa Leo,Anaishi Ilala mtaa wa Mwanza.
Bibi huyu ana hadithi na habari nyingi sana za maisha na siasa,Leo  anaongelea kuhusu ULIMBUKENI!!
Anasema watu wanaharibikiwa sana kwa kukataa yote ya zamani na kuingia kwenye mitindio mipya tuu,kwamba si yote mapya mabaya la! bali na yazamani pia yakumbukwe hasa yale mazuri, Na tuwe tunawafundisha watoto wetu,Asema utakuta mtu kazaliwa na kukulia kwenye familia ya kiswahili lakini mwaka mmoja tuu akienda nje ya nchi,anajifanya kasahau kabisa Kiswahili, mara oohh yah oohh yes, pia hawapendi hata watoto wao wanaowazaa huko au kukulia huko kuwafundisha KISWAHILI, tena na kujisifia wakipiga simu huku nyumbani mwanangu hajui/kasahau kabisa Kiswahili,Kama baba na mama Waswahili iweje mtoto wako asiongee Kiswahili?
Mwisho anawatakia Waislam wote duniani Funga njema yenye baraka na amani.

Nami nasema Ahsante sana bi Zaituni  wa Mrisho na kaka Mtaruke[mjuukuu wa binti Mrisho] yeye ndiye aliyetuunganisha na BIBI huyu.
Haya wapendwa Waswahili neno hilo kutoka kwa bibi unalionaje? Karibuni sana kwa kuchangia,kuelimishana  na.....
Kama una lolote jema na kuelimishana , Unataka kuwaambia Waswahili wenzio karibu  sana unaweza kutumia email hii Rasca@hotmail.co.uk. katika kipengele hiki cha Waswahili na Maisha yao ndani ya Swahili na Waswahili.
Nawatakia Swaumu njema kwa Waliofunga!!