Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Ndoa. Show all posts
Showing posts with label Ndoa. Show all posts

Sunday 1 July 2012

ENGINEER DEUSDEDIT MALULU NA DORIS KASAKA WAMEREMETA KATIKA NDOA YAO TAKATIFU ILIYOFUNGWA JANA.!!!!!


Engineer Deusdedit Malulu akiwa na mke wake kipenzi Doris Joseph Malulu, kwa pamoja wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa Takatifu jana katika kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Mavurunza Kimara.

Engineer Deusdedit Malulu akimvisha pete ya ndoa mke wake mpenzi Doris Kasaka aliyefunga nae ndoa takatifu jana.


Familia ya Mzee Njelu Kasaka wakipiga picha ya kumbukumbu na watoto wao wapendwa Doris Kasaka Malulu na Engineer Deusdedit Malulu waliofunga ndoa takatifu jana jioni.

Maharusi kwa nyuso za furaha wakipiga picha na Mtoto wao.



Engineer Deusdedit Malulu na Mkewe Doris wakikata Keki kwa pamoja kuonyesha kuonyesha ishara ya umoja na mapendo.
Meza kuu ya Familia ya Engineer Deusdedit Malulu

Meza kuu ya Wazazi wa Doris Kasaka.


Engineer Deusdedit Malulu na Doris Kasaka walifunga ndoa takatifu katika kanisa la Katoliki Parokia ya Mavurunza Kimara jana Tarehe 30/06/2012 na baadae kwenye Sherehe ya nguvu iliyofanyka katika ukumbi wa Luxery Mbezi Mwisho.

Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Shirika la ugavi wa Umeme (TANESCO) Makao Makuu na Bi Harusi ni mwajiriwa wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ZANTEL Dar es salaam.


Swahili na Waswahili Tunawatakia Maisha mema yenye Furaha,Amani na Baraka.

Tuesday 21 February 2012

Nderemo na Vifijo Leo -Rwanda, Ni da'Rubango apata Mwenza!!!!!!




















Hayawi hayawi sasa Yamekuwa! dada Rubango na Mumeo Hongereni sana kwa kuwa MKE na MUME!!
Mungu asimamie maisha yenu yawe yenye Baraka na Amani.

UJumbe;dada Rubango na  nawatakia maisha mema yenye Furaha na Upendo wewe na Mumeo,Mungu awenanyi kila iitwapo Leo,Nawapenda sana.
   Wako Neema Nyanyile
      COVENTRY.

Friday 28 October 2011

Mama mkwe Kuvunja Nyumba/Ndoa,ni Mapenzi kwa Mwanawe?Kwani ni Yeye Mama!!

 Wapendwa, hivi kwa nini MAMA MKWE/WAKWE;Hasa  Mama wa MUME.Mara nyingi wanapenda kuiingilia nyumba/Ndoa za watoto wao, Mpaka wengine kufanikiwa kuvunja/kuharibu Mahusiano/Ndoa hizo.Je wanataka mke wanaompenda wao/ kukuchaguli wao au Mapenzi tuu ya Mtoto wake tangu mdogo mpaka Akioa ndiyo yanamfanya aone/waone WIVU?Na JE nini kifanyike ili hali hiyo isitokee?.

Mimi Rachel nasema;Kina mama wakwe watarajiwa na mliokuwa na wakwe tayari,Jamani Taratibu waacheni watoto wajinafasi,Bali pale watakapotaka Ushauri au inapobidi.
Haya nawe Mpenzi Msomaji unalipi la kuongezea au Ushauri,Maoni gani kwa mama Wakwe wa Aina hii?

Karibuni sana Wababa,Wamama,Wanawake na Wanaume,mliokuwa ndani ya ndoa na mliokuwa bado!!!!!!!.

PATA NA BURUDANI YA IJUMAA HII KUTOKA KWA KAKA; MRISHO MPOTO!.